HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 01, 2023

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia katika Maadhimisho ya Sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Dkt. Moses Kusiluka, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya pamoja na Viongozi wengine wakiimba Wimbo wa Mshikamano (Solidarity) wakati wa Sherehe ya Mei Mosi ambazo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wafanyakazi wa Wizara, Sekta mbalimbali za Umma, Binafsi, viongozi pamoja na Wageni mbalimbali katika maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi Kitaifa ambazo zimefanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Wafanyakazi mara baada ya kuhutubia katika Maadhimisho ya Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.
 Kwaya ya Utumishi wa Umma ikitumbuiza katika Maadhimisho ya Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa vyeti, Fedha taslimu pamoja na Makombe kwa Wafanyakazi Hodari pamoja na Wizara zilizoibuka washindi katika michezo ya Mei Mosi 2023 iliyofanyika Mkoani Morogoro

Wafanyakazi kutoka Wizara, Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi pamoja na vitendea kazi vyao wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kutoa ujumbe kuhusiana na masuala mbalimbali ya Wafanyakazi wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.


Viongozi mbalimbali waliohudhuria Maadhimisho ya Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Pages