HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 30, 2023

Tanga yaongoza kwa mvua nyingi, Dar kidogo

 

Na Mwandishi Wetu


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema Mkoa wa Tanga ulipata mvua ya milimita 89.6 iliyonyeesha kwenye mikoa mbalimbali Mei 28,2023.


Imetaja mikoa mingine na kiwango cha mvua kilichopimwa kwenye mabano kuwa ni Kisiwa cha Pemba (67.8mm) kikifuatiwa na Unguja (34.2mm).


Mikoa mingine ni Kilimanjaro (28.0mm) na 

Dar es Salaam (16.5mm) kiwango cha chini kulinganishwa na mikoa mingine iliyotarajiwa kupata mvua siku hiyo.


Februari 22,2023 Kaimu Mkurugenzu Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dk. Ladislaus Chang'a, alitangaza utabiri wa msimu wa mvua za masika zinazonyesha kwenye mikoa inayopata misimu miwili ya mvua  zilizoanza Machi, Aprili hadi Mei (MAM).


Dk. Chang'a alisema maeneo hayo yatapata mvua za wastani hadi chini ya wastani msimu huu wa masika.


Hata hivyo, Aprili 4,2023 Kaimu Meneja wa Ofisi Kuu ya Utabiri TMA, Dk. Mafuru Kantamla, aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kutokana na utabiri walioutoa  kwamba ongezeko la mvua linatarajiwa zaidi kipindi cha Mei na Juni,2023 kutokana na kuimarika kwa mifumo ya utabiri.


Alisema kuimarika huko kumeoneshwa na viashiria vya mfumo wa mvua vinavyoonesha joto la bahari magharibi mwa bahari ya Hindi linatarajia kuongezeka na joto la bahari katika tropiki ya bahari ya Pasific linatarajiwa kuongezeka pia.


Dk. Kantalama alisema ni kawaida mvua za masika kumalizika Mei lakini kipindi hiki zitakwenda mpaka Juni hivyo wananchi na mamlaka mbalimbali ziendelee kuchukua hatua.

No comments:

Post a Comment

Pages