Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Simba inatarajia kumsajili mlinda lango mahiri raia wa Brazil Caique Luis Santos Da Purificacao anayecheza klabu ya Ypiranga Fc
Baada ya kuachana na Beno Kakolanya huku mlinda lango Aishi Manula akitarajiwa kuwa nje kwa miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini, Simba imelazimika kusajili mlinda lango mwingine
Santos mwenye umri wa miaka 25 akiwa amezaliwa Julai 31, 1997 katika mji wa Salvador huko Brazil kwa sasa anaichezea Ypiranga RS inayoshiriki ligi ya Campeonato Brasileiro Serie S, sawa na First League hapa Tanzania akiwa kipa namba moja
Kipa huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 5 alikuwa kwenye akademi ya ES Victory mwaka 2016 kabla ya kuitema na kwenda CSA ya Brazil sambamba na Ermis Aradippou ya Cyprus na Rochester NY ya Marekani kwa nyakati na misimu tofauti
Santos alikuwa kipa namba moja wa timu ya Taifa ya Brazil kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 Brazil (U20) mwaka 2016 na 2017 kikishiriki michuano mbalimbali ya Kimataifa kuonyesha kwamba ni uzoefu wa kutosha
Wakati akiwa kwenye kikosi hicho cha timu ya Taifa alikuwa na nyota wengine wanaowika kwa sasa kwenye soka Duniani akiwemo Richarlison De Andrade wa Tottenham, Douglas Luis wa Astom Villa, Lucas Paqueta wa West Ham na Gabriel Magalhes wa Arsenal
Awali Simba ilihusiswa kumuwania mlinda lango wa Al Hilal Issa Fotana lakini imekuwa ngumu kupata huduma yake baada ya Al Hilal kugoma kumuuza.
No comments:
Post a Comment