NA JOHN MARWA
CHAMA cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) kimetoa rai kwa makapuni na taasisi mbalimbali kujitokeza kuidhamini Ligi Kuu ya Taifa ya Mpira wa Wavu kwa manufaa ya mchezo na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa TAVA Injinia Magoti Mtani, jijini Dar es Salaam ambapo amesema Ligi ya Taifa imekuwa bidhaa hivyo ni vema kwa kamapuni na taasisi kujitokeza kuidhamini ligi hiyo ili kuongeza ubora wa ligi na ajira kwa vijana wa kitanzania.
“Naomba nichukue fursa hii kwa kipekee kabisa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine walitushika mkono katika kuhakikisha Ligi yetu ya Mpira wa Wavu ilifana kwa mwaka jana. Yalikuwa ni mafanikio makubwa hatuweza kubeza na tumepata sehemu ya kuanzia.
“Tunategemea baada ya siku zijazo tukawa na mdhamini rasmi wa hii michuano ambaye tunategemea kumpatia jina la michuano hii, kwa sasa bado jina ni ‘Tanzania Volleyball National League’ (TVNL) hii ndio bidhaa yetu ambayo tunataka tuipatie thamani tuweze kuiuza.
“Tunategemea sana kupitia bidhaa hii ya TVNL kuyabadilisha maisha ya vijana wa kitanzania kupata ajira, kuibadilisha kabisa taswira ya mpira wa wavu Tanzania kuwa ajira kamili. Tunawashukuru sana wale ambao wameendelea kutushika mkono kwa namna ya kipekee sana bila kumsahau mshirika wetu ambaye ni Azam Tv, Lakini na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment