HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 25, 2023

Timu za Taifa Mpira wa Wavu mawindoni, Kocha atajwa

NA JOHN MARWA

MAANDALIZI ya Ligi Kuu ya Taifa Mpira wa Wavu ambayo inatarajiwa kuanza kulindima kesho katika viwanja wa Gwambina jijini Dar es Salaam, yamekamilika ambapo timu zaidi ya ishirini kwa Wanaume na Wanawake kuonyeshana umwamba kumsaka bingwa wa msimu huu.

Akithibitisha kukamilika kwa maandalizi hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) Injinia Magoti Mtani amesema kila kitu kimekamilika hivyo wanatarajia kuwa na ligi bora msimu.

“Maandalizi yanaendelea vizuri, timu zimeashanza kuwasili na mpaka hivi sasa tunategemea jumla ya mechi 10 ambazo zitachezwa siku ya jumatatu juni 26. Mechi ya kwanza itaanza saa moja na nusu ausbui na mechi ya mwisho inategemewa kuanza saa mbili kamili usiku, kwaiyo tutacheza mpaka usiku na burudani itakuwa nzuri sana.

“Ligi hii itahusisha jumla ya klabu 22, kwa msimu huu tunaenda kuwa na ligi ambayo imegusa nchi nzima, mwaka jana hatukupata nafasi ya kupata timu kutoka visiwani Zanzibar lakini mwaka huu tumepata timu tatu kutoka Zanzibar.

“Ambapo moja ni ya kike na mbili za kiume, kwaiyo jumla ya timu 22 zinajumuisha Bara na Visiwani zinakuja kuchuana katika viwanja hivi vya Gwambina.

“Hapa leo tupo katika Viwanja vya Gwambina ambapo ndipo maandalizi yanaendelea kwa ajili ya kuona ni kwa namna gani basi ligi yetu inaweza kufana.


“Tunatoa shukrani za dhati kabisa tutakuwa na mdhamini wetu ambaye pia tulikuwa naye mwaka jana Azam Tv, ambao watahakikisha kuwa watanzania wote wanapata fursa ya kufikiwa na kuangalia burudani hii ya Ligi ya Taifa ya Mpira wa Wavu.” Amesema Injinia Mtani na kuongeza kuwa. 


“Kwaiyo Ligi ya Mpira wa Wavu msimu huu ni wa pili, ni msimu ambao tunauita ni msimu wa maandalizi kwenda kwenye Ligi rasmi. Ukiangalia kwa wale waliopata nafasi ya kuja mwaka jana, tulisema tutakuwa na miaka miwili ya kujitazama, tutaanza na mwaka wa kwanza kuona tunataka nini, lakini tutakuja mwaka wa pili ambao utatupatia picha ya kuona tumekosea wapi tufanye marekebisho.


“Kwaiyo mwaka wa tatu ndio utabeba ile dhima rasmi ya ile Ligi kwa maana ya mizunguko mitano. Mwaka huu tutakuwa na mizunguko mine, tumeongeza mzunguko mmoja kutoka kwenye mwaka uliopita ambao ulikuwa na mizunguko mitatu.


“Kwaiyo mwakani ambapo ni mpango mkakati wetu tumepanga ndio tufanye mizunguko kamili ambayo itakuwa ni Ligi ya mizunguko mitano, kuanzia hapo ligi itakuwa na mizunguko mitano katika misimu itakayofuata.” Injinia Mtani amesema.


“Sasa tunaenda katika mizunguko minne, mzunguko wa kwanza unanza juni 26 kama nilivyosema kwa wiki moja hapa Gwambina, mzunguko wa pili utakuwa mwezi wa saba mwishoni, mzunguko wa tatu utakwenda mwezi wa tisa na mzunguko wa nne nao utakuwa mwezi wa tisa, hiyo ni kwa ajili ya mtoano na fainali.

“Mwezi wa nane unaweza sema kwa  nini umerukwa lakini tutakuwa na ratiba ya kimataifa ambapo timu za Taifa zitakwenda kushiriki michuano ya kimataifa kwa maaana ya timu za Wanawake ma Wanaume.


No comments:

Post a Comment

Pages