HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 29, 2023

WAFANYABISHARA WANAOTUMIA BANDARI WALALAMIKA KUTOZWA KODI MAFUTA YAKIMWAGIKA KWA AJALI

Na Magrethy Katengu

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imelalamikiwa na Wafanyabiashara  kutoka nje ya nchi  wanaofirisha mafuta kwa kutoza kodi mafuta yaliyomwagika baada ya gari kupata  ajali  kitendo ambacho kimewaumiza na kulazimika kuhama kutumia bandari za Tanzania kwenda nchi jirani.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mwinjilisti na mfanyabiashara Alphonce Temba amesema Juni 26 alipokea wageni kutoka nchini Malawi kutoka Kampuni inayohusika kusimamia Magari yote yanayokuja Tanzania kuchukua Petrol magari ambayo yako 200-250, hivyo walikuja kujionea wenyewe kero wanazopata madereva wao wanaposafirisha Mafuta .

Temba amesema walikuja na karatasi waliyokuwa wakilalamikia TRA  kuwa gari yao ilipata ajali Mkoani Mbeya ikitokea Dar es salaam  ambapo Dereva Mtanzania aliigonga kwa nyumba gari ya Dereva Mmalawi na kuichana tanki lake  kisha mafuta yakamwagika askari walipofika eneo la tukio walipima na kuandika karatasi kuwapatia cha ajabu TRA walipofika walipima mafuta yaliyomwagika na  kuyatoza kodi milioni 20 jambo ambalo lilimekuwa likifanyika mara kwa mara na linasikitisha hivyo wakaamua kuja kufuatilia bila mafanikio hivyo wanaiomba serikali iangalie Sheria hiyo ya kodi kwa jicho la tatu inawaumiza wageni.

"Ipo sheria hasa haya magari ya kubeba Petrol na Dizel inayosema kwamba endapo gari hilo linapata ajali kile kilichopotea wanakichukulia kimetumika pamoja na kupewa stakabadhi za polisi wanatoza kodi kwa sababu hakijavuka mpakani hii kodi ipo kwenye Sheria na ni kero kubwa na inamtaka aliyetoa Mzigo kama ni kampuni ilipe tuangalie Mozambique ikitokea kama ajali hiyo Sheria yao inaelekeza lazima aliyemwaga mafuta afanye usafi hilo eneo kama lilivyokuwa mwanzo"amesema Temba

Temba amesema wafanyabiashara wageni idadi yao imepungua kutokana na sheria ya Kodi za holela zisizokuwa na tija hivyo amesisitiza kuwa iangaliwe na hasara anayopata mfanyabishara siyo kuangalia maslahi binafsi tu kwani tunafukuza wafanyabishara wageni


Aidha amelalanikia kitendo cha mamlaka hiyo kuitoza kodi ya milioni 20 kampuni ya Mafuta ya Malawi ya RASHY Motors kutokana na lori lake kumwaga mafuta mara baada ya kupata ajali ya kugongwa kwa nyuma na lori lingine lililokuwa linaendeshwa na dereva Mtanzania katika eneo la Igawilo mkoani Mbeya.

Ameongeza kuwa hali hiyo inasababisha wafanyabiashara wengi kuikimbia bandari za Tanzania na kwenda za nchi jirani ikiwemo Msumbiji ambayo sheria zao ajali kama hiyo ikitokea wajibu wa mfanyabiashara ni kusafisha barabara na mafuta yaliyomwagika hayatozwi kodi huku Tanzania ikiyahesabu mafuta hayo kuwa yametumika nchini hivyo yalipiwe kodi.

“Wafanyabiashara wa Malawi wanapenda kupitisha mafuta yao hapa nchini kutokana na ubora wa barabara za Tanzania kuliko Msumbiji hivyo kama sheria za TRA hazitarekebishwa tutegemee wafanyabiashara wa nchi wakiendelea kupungua” Amesema Bw. Temba.

Hata hivyo amesisitiza serikali kuangalia upya suala hilo kwa kurekebisha sheria za TRA  kwani kuendelea kuzitumia kutawakimbiza wafanyabiashara na kuikoseha serikali mapato.


No comments:

Post a Comment

Pages