HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 29, 2023

AZAM FC YAMSHUSHA WINGA KUTOKA RAJA CASABLANCA

Na John Marwa

Klabu ya Azam FC imemtambulisha kiungo mshambuliaji Djibril Sillah raia wa Gambia kutokea Raja Casablanca ya Morocco.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na klabu ya Azam FC jioni ya leo katika mitandao yao ya kijamii imeeleza kuwa wamemnunua nyota huyo kuja kuongeza nguvu katika kikosi chao.

""Tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefikia makubaliano na klabu ya Raja Casablanca, ya kumnunua kiungo wao mshambuliaji, Gibril Sillah.

"Nyota huyo wa Gambia, anatarajia kutua nchini muda wowote kuanzia sasa kumalizia taratibu za mwisho za usajili.

"Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu ya Morocco, Sillah alifanikiwa kufunga jumla ya mabao saba na kutoa pasi za mwisho nne, wakati akiwa kwa mkopo JS Soualem." Imeeleza taarifa hiyo.


No comments:

Post a Comment

Pages