HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 13, 2023

ACB BENKI KUJIKITA KULETA MAPINDUZI YA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE


 Na Mwandishi wetu

Akiba Commercial Bank Plc( ACB) imesema itahakikisha  inaendelea kujikita kuleta mapinduzi ya utoaji  huduma bora za kibenki hapa nchini kwa  kuboresha  huduma zake ikiwemo kuweka fedha na kutoa fedha pia kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa . 
Akizungumaza Jijini Dar es salaam na  Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc,  Silvest Arumasi wakati katika banda la benki hiyo katoka maonyesho ya  ya  47 ya Sabasaba ndani ya amesema kuwa benki ya Akiba imeboresha huduma zake ambazo zitakuwa chachu  ya  kukidhi matarajio ya wateja waliopo pamoja na wateja watarajiwa katika kujipatia huduma. 

Hata hivyo amebainisha kuwa Maboresho makubwa yamefanywa kwa huduma za wateja binafsi,(Personal banking) ambayo inawalenga Waajiriwa wa sekta za Umma na sekta binafsi ambapo  mteja anaweza kupata mikopo  ya aina mbalimbali kuendana na mahitaji yake mathalani huduma za mikopo ya kujenga na kuboresha makazi, pia mikopo ya muda mfupi (Salary advance) kwa ajili ya kutatua dharura za kifedha kwa muda mfupi. 
" Benki imezidi kuboresha huduma za mikopo kwa wateja wakubwa ,w (Corporate customers) wakati,na wadogo kuendana na mahitaji ya soko na tunatoa huduma za bima kwa wajasiriamali pamoja na vikundi mbalimbali ikiwemo mikopo ya bima –IPF (Insurance Premium Financing)" amesema Mkurugenzi

 Sambamba na hayo Mkurugenzi amebainisha  kuwa benki imeboresha huduma zake  kwa kupitia Mawakala wake  (Akiba Wakala) na simu ya mkononi (Akiba Mobile) pia  imeboresha mifumo ya utumaji pesa kwenda nje ya nchi.

 Aidha  wito umetolewa kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo na  amewashukuru kuchagua benki ACB hiyo kutumia huduma zake  ikiwemo wafanyakazi ,Wajasriamali hivyo amewasisitiza waendelee kupata huduma bora kwani ni benki sahihi na bora inayolenga kutimiza malengo ya Wateja wake.

No comments:

Post a Comment

Pages