HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 13, 2023

NBC kuwanoa elimu ya kifedha wafanyakazi 3,600 Muhimbili

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekubali ombi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH-Upanga & Mloganzila) la kutoa elimu kwa wafanyakazi wake 3,600 juu ya masuala ya kifedha, fursa mbalimbali zilizopo na vihatarishi vyake ili waweze kuchukua hatua stahiki kabla ya kukopa au kuwekeza.


Ahadi hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi (Maalum) kutoka NBC Makao Makuu, Bi. Ashura Waziri alipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi ili kujadiliana naye kuhusu masuala mbalimbali na fursa za ushirikiano.


Kwa upande wake Prof. Janabi amesema, pamoja na mambo mengine, ameiomba Benki hiyo kusaidia kutoa elimu kwa wafanyakazi kuhusu masuala ya kifedha ili kuwaepusha na msongo wa mawazo pale ambapo mategemeo yao yanaenda kinyume na matarajio baada ya kukopa au kuwekeza.


“Ningependa kuona wafanyakazi wakikopa mahali sahihi, kwa utaratibu sahihi na kujiepusha na mikopo ya haraka haraka kwani baadhi yao inawaletea changamoto kubwa pale wanaposhindwa kulipa kwa wakati, kupata msongo wa mawazo na kushindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu” amesisitiza Prof. Janabi.

No comments:

Post a Comment

Pages