HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 24, 2023

Chuo Kikuu Mzumbe chajivunia mafakinio

Naibu Waziri wa Elimu, Omary Kipanga (kushoto) akimkadhi cheti Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, wakati wa kilele cha Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Mipango Utawala na Fedha, Prof. Allen Mushi (kushoto) akipata maelezo wakati alipotembelea banda la chuo hicho wakati wa kilele cha Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.

Wananchi wakipata huduma katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Mipango Utawala na Fedha, Prof. Allen Mushi (kushoto) akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa chuo hicho wakati wa kilele cha Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Kaimu Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (katikati), akiwa katika picha ya kumbukumbu alipotembelea banda la Chuo hicho wakati wa kilele cha Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Chuo Kikuu Mzumbe kimehitimisha Maonesho na kujivunia kutoa wahitimu wengi ambao kwa sasa ni viongozi wakubwa Serikalini.

Akizungumza kwenye maonyesho ya 18 ya vyuo vikuu Kaimu Makamu chuo kikuu Mzumbe  Prof. William Mwegoha amesema udahili umekuwa ukiongezeka kila mwaka ni kutokana na matokeo ya juhudi ambazo wanazifanya timu nzima,ya chuo katika kuushawishi Umma kuwa wanatoa program nzuri zinazotoa matokeo mazuri ikiwemo upande wa Sheria.

"Kwa upande wa Sheria tunafundisha kwa vitendo kwa vitendo na hata vijana wanapokwenda kwenye Shule ya Sheria Yaani Low School, ni kati ya vijana ambao wanafanya vizuri sana kuanzia program yetu ni miaka mitatu ikilinganishwa miaka minne ambayo vyuo vingine vyote vinatoa lakini wanafunzi wanaotoka Mzumbe ni Wazuri zaidi kwa vitendo na uwezo wa kufanya kazi.

Lakini maeneo mengine ambayo tupo vizuri ni upande wa utawala ambapo ni kati ya nguzo muhimu sana ni kufundisha viongozi upande wa Rasilimali watu, upande wa usimamizi na utawala ambao kutokana na aina yetu ya ufundishaji ambapo wanafunzi wanakwenda kwenye mafunzo ya vitendo wanakwenda kwa muda mrefu,hivyo basi wanajenga uwezo wa ufanyaji wa kazi hata kabla ya kumaliza chuo,hivyo wakitoka hapo inakuwa ni rahisi sana kupata ajira kwa sababu wanachukuliwa sana kwa ajili ya kujitolea na kupitia huko wanapata ajira amesema,"Prof. Mwegoha.

Amesema kwa upande wa wa mahusiano mazuri waliyoyajenga kwenye makampuni,Viwanda na Taasisi mbalimbali ambazo zinachukua wanafunzi wao kwa ajili ya kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo baada ya kutoka wanakuwa tayari kuingia kwenye soko la ajira au kujiajiri.

Maonyesho hayo ya 18 ambayo yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)  yalifunguliwa Julai 17, 2023, yamehitimishwa Julai 22, 2023  na Naibu Waziri Omary Juma Kipanga.

No comments:

Post a Comment

Pages