Mkurugenzi wa Hazina Bw. Wenceslaus Fungamtama, akikata utepe kuzindua majengo mapya ya vyoo vya Shule ya Msingi Kikelelwa iliyopo Rombo mkoani Kilimanjaro. Majengo hayo yamejengwa na Benki ya TCB. Wa pili kulia ni Afisa Elimu Idara ya Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Alice Makule na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Charles Amos.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kikelelwa wakifurahia matumizi ya majengo yaliyojengwa chini ya ufadhili wa TCB.
Na Mwandishi Wetu
Zaidi ya wanafunzi 700 katika Shule ya Msingi Kikelelwa iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wamesaidiwa kuondokana na changamoto ya hatari ya kuambukizana magonjwa mbalimbali ikiwemo kipindupindu hivyo wamepata msaada wa kujengewa matundu ya vyoo 18 na benki ya Taifa ya biashara (TCB) ambapo hapo awali walikuwa wanatumia vyoo chakavu na matundu machache.
Akizundua vyoo hivyo shuleni hapo Mkurugenzi wa Hazina Tanzania Commacial Bank Wenceslaus Fungamtama kwa niaba ya Afisa mtendaji mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi amesema lengo la kujenga vyoo hivyo ni ili kuboresha mazingira na utulivu wa kujifunza kwa wanafunzi hao wawapo shuleni na wasikumbane na changamoto ya magonjwa ya kuambukizana.
"Ili kuunga jitihada za serikali za kuboresha huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu, benki ya TCB hutenga kiasi cha zaidi ya milioni milioni 300 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu zimeweza kujenga madarasa, nyumba za walimu na vyoo katika maeneo mbali hapa nchini" amesema Fungamtama.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Charles Amos ameshukuru benki hiyo kwa kusaidia ujenzi wa matundu ya vyoo kwani mesema kutokana na uchache wa matundu ya vyoo yaliyokuwepo awali wanafunzi walilazimika kupanga foleni ya kusubiriana huku wale wadogo kujikojolea.
"Tunawatoto waliokuwa wanatoroka kwenda nyumbana kwa aibu ya kujikojolea, hasa muda wa mapumziko ambao wanatoka darasani kwa pamoja, lakini sasa kwa vyoo hivi ni wazi kutakuwa na utulivu wa kujifunza" amefafanua Mwl.Amos
Dada mkuu wa shule hiyo Careen Jonas ameonyesha furaha yake kuwa licha ya vyoo hivyo kujengwa kisasa, vikizingatia miundombinu ya walemavu lakini pia vina chumba maalumu cha kubadilishia nguo kwa waschana wawapo kwenye siku zao za hedhi.
Kwa upande wake Afisa elimu idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Rombo Alice Makule, amesema hivi sasa shule inajumla ya wanafunzi 768, wavulana 385 na wasichana 378 ambapo kwa uwiano ilitakiwa kuwe na matundu 16 kwa wavulana na 19 kwa wasichana lakini wakitumia matano matano tu hivyo ujio wa benki hiyo kujenga matundu 18 umepunguza tatizo kwa kiasi kikubwa.
Shule ya msingi Kikelerwa ambayo ipo mpakani mwa Tanzania ni moja kati ya shule kongwe za Mkoa wa Kilimanjaro, licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo uchakavu wa madarasa vyoo na uchache wa walimu lakini imeendelea wa kufanya vizuri kitaaluma kiufaulu.
No comments:
Post a Comment