HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 24, 2023

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA TATU, KARATE MAZIWA MAKUU

Na Mwandishi Wetu


Timu ya Taifa ya mchezo wa Karate imeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya Maziwa Makuu yaliyoanza Julai 21, 2023 na kumalizika Jana Julai 23, 2023.

Katika Mashindano ya mwaka huu Nchi 12 za Maziwa makuu zilifanikiwa kushiriki na Mgeni mualikwa ilikuwa ni nchi ya Cameroon ambayo ilikuwa Nchi ya
13 kwa idadi ya jumla.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Jerome Mhagama
Katibu Mkuu Tanzania Sports Karate-Do Federation (TSKF) imeeleza kuwa Tanzania Imefanikiwa kkujikusanyia Medal 45 katika mashindano hayo.

"Timu yetu imefanikiwa kujikusanyia Medali 45 katika Mashindano haya ya mwaka huu, na hii imetufanya kama Nchi kuwa Washindi wa tatu kwenye ushindi wa jumla ya matokeo yote tukitanguliwa na Cameroon na Wenyeji Congo.

"Katika mashindano haya kulikuwa na Makundi (categories) 22 zikiwemo Women’s Team Kata & Individual Kata, Men’s Team Kata & Individual Kata, Women’s Team Kumite & Individual Kumite, Men’s Team Kumite & Individual Kumite.

"Tanzania tulikuwa na wachezaji katika kila kundi (category)kwa pande zote mbili kwa Wanawake na Wanaume yaani Cadet miaka 14-15, Junior miaka 16-17 na Senior miaka 18 na Kuendelea." Amesema na kuongeza kuwa.
 


"Sambamba na hilo, Wachezaji wetu wamefanikiwa kumaliza katika nafasi tatu za juu kutoka katika kila kundi (category). Katika makundi (category) 2  tumechukua nafasi ya Kwanza (1st Place), makundi (category) 4 tumechukua nafasi ya Pili (2ndPlace) na  Makundi (categories) yaliyobakia tumeshika nafasi ya Tatu (3rdPlace).

"Kwa matokea haya yanatufanya Tanzania kuwa na medali kama ifuatavyo;  
1.Gold Medals-2
2.Silver Medals-7
3.Bronze Medals-36

"Kwa ujumla Mashindano ya mwaka huu yalikuwa na ushindani mkubwa sana, na nachukua nafasi hii kwa niaba ya Tanzania Sports Karate-Do Federation (TSKF) kuwapongeza Vijana wetu, Viongozi walioambatana na timu kwa kulipambania Taifa kwa Nidhamu,Juhudi, Maarifa, Weledi na Uzalendo uliotukuka." Hata hivyo amebainisha kuwa.

"Hakika tunajivunia kuipeperusha vyema Bendera yetu nakuipa
heshma Nchi yetu pendwa ndani na nje ya mipaka yetu.


"Pia tunaishukuru Serikali yetu inayoongozwa na Mama yetu Mpendwa Mhe. Dr.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusaidia kutoa usafiri maalum wa kwenda na kurudi kwa Timu yetu.

"Pia tunaishukuru Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri wetu Dr. Pindi H. Chana, Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu Bw. Said Othman Yakubu,  Bw.Ally Mayayi Tembele Kaimu Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Michezo na wafanya kazi wote wa Wizara.

"Na kwa upekee Tunalishukuru Baraza La Michezo Tanzania (BMT) chini ya Bw. Leodegar Tenga Mwenyekiti wa Bodi, Bi. Neema Yotham Msitha Katibu Mtendaji BMT na wafanya kazi wote wa Baraza kwa mchango mkubwawa muda  wote kwa Timu hii na maendeleo ya mchezo wa Karate nchini." Amesema Mhagama na kueleza kuwa.

"Timu inatarajia kuanza safari ya kurudi nyumbani kesho (Leo) Julai 24, 2023 majira  ya saa 04:00 asubuhi kwa saa za Congo, na tunatarajia itafika nyumbani  Tanzania siku ya jumatano kuanzia majira ya saa 10:00 jioni." Amesema

Nchi washiriki katika mashindano hayo zilikuwa ni Angola, Burundi, Central African Republic, Republic of Congo,
Kenya, Uganda, Rwanda, Republic of South Sudan,Sudan, Tanzania, Zambia, Democratic Republic of Congo, Cameroon.
 

No comments:

Post a Comment

Pages