HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 21, 2023

DC TEMEKE ATOA SIKU 25 MKANDARASI KUKABIDHI SOKO LA ZAKHEM KWA MANISPAA YA TEMEKE

Na Khadija Kalili

MKUU wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa  Mobhare Matinyi  leo Agosti 21 ameridhishwa na hali ya ujenzi wa soko jipya na la Kisasa lililopo Mbagala Kibonde Maji  (Zakhem)  huku akimtaka mkandarasi wa soko hilo kulikabidhi kwa Manispaa ya Temeke  ifikapo Agosti 15 ,2023.

Awali ya yote nachukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri  ya Muungano  wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa kutoa  fedha kiasi cha  Bil.2.843  ambazo zimejenga soko hili jipa na  la kisasa  ndani ya Manispaa ya Temeke, nachukua fursa hii  kusema kuwa baada ya mkandarasi kukabidhi soko hili kazi inayobaki ni kwa Mkurugenzi Elihuruma Mabelya wa Manispaa  ya Temeke,  Mstahiki  Meya wa Manispaa  ya Temeke Abdalah Mtinika  pamoja na Katibu  wa wafanya biashara katika  soko hili waketi pamoja na kupanga  namna wafanyabiashara watakavyo pangwa ndani ya soko huku kipaumbele kikiwa ni kwa wale wafanyabiashara ambao walikuwepo awali wakati wa lile soko duni.


"Viongozi mtatakiwa  kusimamia mgawanyiko   wa vizimba vya biashara  kulingana na  ukubwa wa biashara " amesema Matinyi.


Pia  jumla ya  mamalishe 20 waliokuwepo awali watapewa kipaumbele ndani ya soko hilo, amesema Mheshimiwa Matinyi.
Amesema kuwa ujenzi wa soko hilo umechukua muda wa mwaka mmoja  kikamilifu  ambapo awali kulikua na soko duni ambapo hivi sasa  kuna  vizimba 160 hukumiundo mbinu ikiwa  ni rafiki  na kufikika kwa urahisi kwa ujumla.

Katika soko hili kutakua na ofisi za Manispaa ambao watasimamaia masuala.ya msingi ndani ya soko pia kutakuwa na kitengo cha Tehama ambacho kitafunga mitambo maalumu ili kufuatilia nyendo zote za wafanyabiashara na utendaji wao kazi  ndani ya soko, huku ametoa onyo kali kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa wafanyabiashara ambao watafanya uhuni  endapo watapangishwa  kwa fedha ndogo ya serikali  halafu na wao wapangishe wafanyabiashara wengine.


Wakati huohuo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya  amesema kuwa wamejipanga kuwaondoa wafanyabiashara ambao huzagaa hovyo pembezoni mwa barabara kwa kuwa wanakwenda kinyume na sheria huku akisisitiza kwa kusema kuwa Manispaa hiyo  wamejipanga  na wataanzisha kampeni ya kuwaondoa pamoja kuiweka Temeke safi kwa ujumla.

 
"Tumetenga kiasi cha Bil.1 ambazo zitafanya ukarabati wa masoko ndani ya Manispaa ya Temeke huku amesisitiza  kwa kusema kuwa wafanyabiashara  wanaokaa pembezoni  mwa barabara si wa Dar es Salaam  pekee  bali nchi nzima wanakua sawa na uchafu kutokana na kuzagaa hovyo hivyo wamejipanga kuanzisha kampeni ya usafi ndani ya Manispaa ya Temeke itakayoanza hivi karibuni na kutekelezwa usiku na mchana.


No comments:

Post a Comment

Pages