HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 21, 2023

JEZI MPYA YA SIMBA SC GUMZO KILA KONA

Na John Marwa


Hatimaye klabu ya Simba imemtanbulisha jezi mpya za msimu ujao wa mashindano 2023/24 kama ambavyo walieleza hapo awali kuwa usiku wa leo zinatambulishwa mara baada ya kibegi cha jezi hizo kufikishwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Safari ya kupeleka jezi hizo Mlima Kilimanjaro ilianza juzi na leo saa moja usiku waliokkabidhiwa jukumu la kuzipandisha na kuzindua jezi wmmefika kileleni na kufanya zoezi hilo.

Simba wamemtambulisha jezi aina tatu, jezi ya nyumbani ambayo ni nyekundu, jezi ugenini ambayo ni nyeupe huku jezi ya bluu yenye michrizi mieupe na miekundu ikiwa jezi ya ziada ama 'third kit'.

Jezi hizo zimekuwa gumzo kila kona ya vijiwe vya kidijitali ambako wapenzi, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wameonyesha kukubaliana na uzuri na ubora wake kwa kuzimwagia maua na kumzifia mzabuni mpya wa vifaa vya michezo Sandaland 'The Only One'.

Jezi ya bluu imeonesha kuwateka wengi kwa jinsi ilivyo na nakshi nakshi zake huku wengine wakionyesha kuzikubali jezi zote tatu.

Wakati huo huo majibu ya ni jezi za akina nani zilikuwa kwenye kibegi ambacho kimetawala vijiwe vya kidijitali hasa mtandao wa Twitter ni jezi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na Rais wa heshima wa klabu ya Simba Mohamed Dewji 'Mo Dewji'.

Licha ya kuzikubali jezi hizo wapenzi mashabiki na wanachama wameanza kuzishambulia usiku huu katika miji mbalimbali hapa nchini.



No comments:

Post a Comment

Pages