Watanzania
wameshauriwa kutoogopa kuwapeleka watoto wao kusoma Vyuo Vikuu vya Nje
ya Nchi kwa kuhofia gharama kubwa za mahitaji mbalimbali ikiwemo ada na
fedha za kujikimu badala yake wawapeleke ili wapate elimu bora
inayoendana na soko la dunia.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Education link,[GEL]
Abdulmalik Mollel alipokuwa akimwelezea Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Prof Adolf Mkenda wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo
katika ufunguzi wa Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia
yenye kauli mbiu isemayo "kukuza elimu nchini kupitia elimu ya
juu,sayansi na teknolojia kwa uchumi imara na ushindani"yanayofanyika
katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 17
hadi 22 mwaka huu.
Amesema
kampuni hiyo inayojihusisha uwakala wa kupeleka wanafunzi kusoma nje ya
nchi ina vyuo bora 14 vya gharama nafuu ikiwemo katika nchi za
Uturuki,India,Canada na Malawi ambapo amesema wanatamani waone sylabus
za kitanzania zikifundishwa katika vyuo hivyo.
Abdulmalik
amebainisha kuwa mfano vyuo vikuu bora vya nchini India ambavyo
hufundisha masomo ya uhandisi kwa gharama nafuu,Abulmalik amesema
mwanafunzi anayepata bahati ya kujiunga na vyuo hivyo hutumia dola 510
kwa ajili ya chakula mwaka mzima huku ada ikiwa ni dola 1500 ambayo
mtanzania anaweza kumgharamia mwanafunzi kwa kulipa kidogo kidogo mpaka
mtoto wake atakapohitimu mafunzo yake.
"tunatamani
mafunzo ya kozi za uhandisi wanafunzi waweze kwenda kusoma nje ya nchi
ili wapate teknolojia mpya hivyo tunaweza kuwaomba wazazi wawalete
watoto wao hapa glaballink ili tuwafanyie udahili na wasiogope
kiingereza kwani ni sawa na kile walichofundishwa mashuleni hapa
nchini"amesema
Maonesho
hayo ya elimu ya juu yanafanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam huku kampuni ya Global Education ink ikiwa ni moja ya makampuni
ynayoshiriki maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment