HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 21, 2023

Mnyama aendelea kushusha vyumaa

Na Mwandishi Wetu

Klabu ya Simba imeendelea kushusha vyumaa ikiwa ni muendelezo wa kuboresha kikosi kuelekea msimu ujao.


Simba katika moja na mbili siku ya leo wametangaza wachezaji watatu wapya wazawa ambapo wametangaza Mshambuliaji Shaban Chilunda ambaye aliachana na Azam FC baada ya msimu kumalizika.

Chilunda amewahi kukipiga pia nchini Hispania kunako timu ya Ligi ya Daraja la kwanza.

Mnyama Simba wamemtambusha kiungo wa Dimba la chini Abdallah Hamis amejiunga na Simba akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Opara United ya nchini Botswana kumalizika.

Hamis ambaye ni Mtanzania ana umri wa miaka 24 amewahi kupita klabu za Sony Sugar, Bandari Fc za nchini Kenya.

Mchezaji mwingine wamemtambulisha Hussein Kazi ni beki wa Kati amejiunga na simba akitokea Geita Gold na yeye ni Mtanzania.



No comments:

Post a Comment

Pages