HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 21, 2023

JET yasisitiza habari za uhifadhi wa bioanowai

  

Na Selemani Msuya, Bagamoyo


CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kimetoa raia kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini kuhamasisha waandishi kuandika habari za uhifadhi wa bioanowai.


Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa JET, Dk Ellen Otaru wakati akizungumza na wahariri wanaoshiriki mafunzo ya siku mbili kuhusu hifadhi ya bioanowai kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, mafunzo yanayoratibiwa na JET na kufadhiliwa na USAID Tuhifadhi Maliasili.


Amesema lengo la JET kukukutana na wahariri ni katika kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa mambo ya uhifadhi wa bioanowai na mazingira, hali ambayo itawafanya wahamasishe waandishi kuandika habari hizo kwa wingi.


"JET imetoa mafunzo ya uhifadhi wa bioanowai kwa waandishi wa habari, hivyo katika kuhakikisha jambo hili linakuwa ajenda ya vyombo vya habari tumelazimika kuwapa mafunzo wahariri ili nao wapate uelewa na wanapoletewa kazi za uhifadhi wazipe kipaumbele," amesema.


Mwenyekiti huyo amesema JET inaamini iwapo wahariri watafundishwa faida za bioanowai watakuwa sehemu ya kampeni ya kufanya mazingira  na shoroba yawe salama na endelevu.


Amesema jamii inahitaji kupata taarifa sahihi kuhusu uhifadhi wa bioanowai na mazingira, hivyo kupitia mafunzo hayo kwa wahariri wanaamini lengo litatimia.


Dk Utaru amesema wahariri na waandishi wanapaswa kuelimisha jamii kuwa suala la uhifadhi wa bioanowai na shoroba ni jukumu la kila mtu kwani madhara yake hayachagui.


Mjumbe wa Bodi ya JET, Bakari Kimwanga amesema  chama hicho kupitia ufadhili wa USAID Tuhifadhi Maliasili wanatekeleza mradi katika shoroba saba, hivyo wanaomba waandishi na wahariri kuwaunga mkono katika kampeni hiyo inayolenga kulinda rasilimali za nchi.


Kimwanga amesema ombi la JET kwa wahariri kutoa kipaumbele kwa kila habari inayohusiana na uhifadhi wa bioanowai ambayo itawasilishwa kwenye dawati.


"Ninachowaomba ndugu zangu habari yoyote ya uhifadhi wa bioanowai msiiache kwani hali ni mbaya kwa sasa na sisi JET tutandelea kukutana nanyi ili tukumbushane," amesema.


Mkurugenzi w JET, John Chikomo amesema ushirikiano ambao wanapata kwa vyombo vya habari umechangia wafadhili wa mradi ambao ni Marekani kuahidi kuwapatia fedha za utekelezaji.


Chikomo amesema mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili unapaswa kupongezwa kwa kuwa umeanza kutoa matokeo chanya.



No comments:

Post a Comment

Pages