HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2023

TPDC NA MPANGO WA GESI MAJUMBANI WAJA

 
Mussa Mohamed Makame, akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2023 kuhusu mafanikio na mikakati ya shirika hilo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Francis Mwakapilila, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Derick Moshi na kushoto ni Mkurugenzi Utafutaji na Uendelezaji wa Gesi Asilia, Kenneth Mutaogwa.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile, akizungumza katika mkutano wa Wahariri na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu mafanikio na mikakati ya shirika hilo.
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Derick Moshi.
Mkurugenzi wa Biashara ya Petroli, Mpambika Chiume, akizungumza katika mkutano huo.

 


Na Mwandishi Wetu

 

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linaendelea na ujenzi wa kituo Mama cha usambazaji wa gesi huku kikitarajiwa kuratibu shughuli nyingi za kushindilia, kupakia na kusambza gesi katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame, amesema suala la matumizi ya gesi kwenye magari na nyumbani katika jiji la Dar Es Salaam, ujenzi wa kituo mama unaendelea.

 

“Suala la matumizi ya gesi kwenye magari na majumbani hapa jijini Dar es Salaam ambapo sasa hivi mradi tunaoutekeleza ni mradi ule wa kujenga kituo mama cha usambazaji wa gesi iliyoshindiliwa, kinajengwa katika eneo la Mlimani City maeneo ya Ubungo, kile kituo chenyewe kitakuwa kinafanya kazi nyingi. 

 

“Cha kwanza kitakuwa kinashindilia gesi, ili itiwe kwenye malori ambayo yatakuwa yanapelekwa kwenye vituo dada ambavyo vitakua nje ya pale lakini pia kitakuwa kinajaza magari palepale mlimani city. Kwa sasa vituo viwili ambavyo vitakuwa vinapokea kutokea pale, kimoja kitakuwa Kibaha karibu na kiwanda cha Madawa cha Kairuki, kingine kitakuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 

“Tutakuwa na vituo vingine ambavyo vitajengwa na kampuni binafsi ambazo tumeingia nazo makubaliano, moja inaitwa Tata Arabia wao wameshaanza ujenzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kmbarage Nyerere, kituo kingine nao watajenga barabra ya Samnajoma mjini.” amesema Makame na kuongeza kuwa.

 

“Kwa sasa kingine tunachokifanya ni kutengeneza mpango mkakati wa kusambaza gesi kwenye mji mzima wa Dar es Salaam pia kuitoa nje ya Jiji la Dar es Salaam. Huu mpango tunategemea utachukua miezi minne mpaka sita utakuwa tayari tutatoa maelekezo yake, vilevile ndio utawezesha wale wawekezaji ambao wamechukua idhini kwetu kwenda kuwekeza, kuweza kujua ni eneo lipi zuri, soko lake limekaaje ili waweze kuwekeza kwenye maeneo hayo.

 

“Vilevile tutaangalia kwenye barabara kuu zote za Jiji la Dar es Salaam, kama mnavyojua barabra ya Bagamoyo. Morogoro, Kigamboni, Kisarawe na Barabara ya kuelekea Lindi au Kilwa zote tuhakikishe kwamba kila kona ambayo inaingia katikati ya Jiji iwe imepata vituo vya kusaambazia gesi. 

 

“Kwaiyo, hiyo ndio mipango ya muda mfupi, lakini mipango ya muda mrefu ni kuangalia namna ambavyo gesi itafika mpaka nje ya Dar es Salaam, tukianza na njia ya kati kuanzia Morogoro mpaka Dodoma na njia nyinginezo za Kaskazini na kwenda kusini  ambayo pia inapitiwa na Bomba lile kuu, pamoja na njia ya kuelekea mikoa ya nyanda za juu kusini.” Amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages