HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 24, 2023

SIMBA SC YAMPIGA BEI SAKHO, UFARANSA

 


Na John Marwa

Klabu ya Simba imetangaza kumuuza mchezaji wao nyota wa Senegal Pape Sakho kwenda klabu ya Quevilly Rouen Metropole ya Ufaransa.

Sakho ameitumikia Simba katika misimu miwili huku mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa Simba ni kushinda kiatu cha Bao bora la msimu wa mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

"Simba SC tumefikia makubaliano na Klabu ya Quevilly Rouen Metropole ya nchini Ufaransa kumnunua mchezaji wetu Pape Sakho.  Tunamtakia kila la kheri Sakho kwenye timu yake." Simba SC.

No comments:

Post a Comment

Pages