HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 17, 2023

WAJELAJELA WAANZA NA KIHIMBWA

Na Mwandishi Wetu 


Uongozi wa Klabu ya Tanzania Prisons Sc umeingia mkataba wa mwaka mmoja na  mchezaji Salamu Ramadhani Kihimbwa.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo asubui ya leo imeeleza kuwa Kihimbwa ataitumikia Tanzania Prisons kwa  mwaka mmoja.


"Kihimbwa ataitumikia timu yetu katika mashindano yote tutakayo cheza msimu ujao wa 2023-2024.


"Kabla ya kujiunga na timu yetu Kihimbwa alikuwa mchezaji wa Mbeya City Fc msimu uliyopita 2022-2023." Imeeleza taarifa hiyo.


Usajili wa Kihimbwa unakuwa wa kwanza kwa wajelajela, wakianza kiimarisha eneo lao la ushambuliaji.

No comments:

Post a Comment

Pages