HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 29, 2023

ZFF KUKAA KITAKO NA CECAFA KUKUZA SOKA LA ZANZIBAR


Na John Marwa


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Visiwani Zanzibar (ZFF), Sulaiman Jabir amsema  wako kwenye mchakato wa kuzungumza na viongozi wa CECAFA, ili timu za visiwani humo  kuwa  sehemu ya kalenda ya michuano ya ukanda huo Ili ziweze kuwa timu shindani katika michuano ya kimataifa.



Ameyasema hayo mara baada ya timu ya Visiwani humo ya Wasichana U-18 kuanza vibaya katika mashindano ya kuwania ubingwa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, (CECAFA U-18) kwa kukubali kichapo cha mabao (3-0) dhidi ya Uganda.


Akifanya mahojiano maalumu na Habari Mseto, Rais Jabir amesema timu yake ilicheza vizuri kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuzuia goli lao kwa sababu ya kutokuwa na uzoefu katika mashindani hayo.


Amesema timu yao haina uzoefu mkubwa na kulazimika kukutana na viongozi wa CECAFA kutaka timu za wasichana, wanawake na vijana kutoka Visiwani Zanzibar kuingia katika kalenda yao.


“Ili kuimarisha soka la wanawake Zanzibar na vijana kuwa na ushindani zaidi, tunaomba CECAFA kuwa sehemu ya kalenda yao kwa timu hizo kwa ajili ya kupata mechi nyingi za  michuano ya kimataifa,” amesema Rais Jabir.


"Tukibahatika kuingia katika kalenda hiyo timu zetu zitapata mechi za kimataifa na kupata uzoefu mkubwa na kuweza kuwa tishio kama zilivyokuwa nyingine,” ameema Rais huyo.


Amebainisha kuwa,  wako katika mchakato wa kuendelea kuimarisha  timu za Taifa za wanawake visiwani humo kwa katafuta michezo ya kimataifa ya kirafiki ambayo itawafanya kuwa na timu imara kwa hapo baadae.


“Bahati nzuri siku hizi kuna mashindano ya mashule na tayari tumeandaa programu ya muda mrefu  na tunampango wa kuipeleka Wizara ya Elimu ili kuhakikisha tunaimarisha soka la wanawake, vijana na walemavu,” amesema Rais Jabir.


Kuhusu muelekeo ya timu yao katika mashindano ya CECAFA U18 WOMEN'S CHAMPIONSHIP, amesema licha ya kupoteza mechi ya kwanza bado anaimani kubwa na vijana wake wanaweza kufanya vizuri katika michezo inayofuatia.


“Nimefanikiwa kuongea na wachezaji wangu na wamedai wanasahau matokeo ya mechi iliyopita na sasa nguvu zao wanazielekeza katika mechi ijayo dhidi ya Tanzania Bara.” amesema Rais Jabir.

No comments:

Post a Comment

Pages