HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 25, 2023

CBE YA ETHIOPIA YATINGA NUSU FAINALI CECAFA

CECAFA - Uganda
 
Timu ya Wanawake ya CBE FC ya Ethiopia imefuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano ya CECAFA kuwania kufuzu Fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake yanayoendelea hapa Jinja, nchini Uganda.

CBE imemaliza ikiwa vinara katika kundi A hatua ya makundi ikiwa na alama 10 baada ya leo, August 24, 2023 kuifunga timu ya Yei Joints Star magoli 4-0.

CBE itacheza nusu fainali na mshindi wa pili katika kundi B, Vihiga Queens mchezo ambao utachezwa August 27, 2023 kuanzia saa 9:00 jioni katika uwanja wa FTC - Njeru.


No comments:

Post a Comment

Pages