HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 25, 2023

KIJANA MZALENDO AJITOKEZA HADHARANI KUTOA USHAURI KWA TAASISI ZA KIDINI SUALA LA BANDARI

Na Magrethy Katengu

Kijana Mzalendo wa Kitanzania Ahmed Kombo ajitokeza hadharani kuziomba Taasisi za Kidini kutoingilia masuala ya kisiasa hususani Sakata la Bandari linaloendelea wasije sababisha machafuko au ubaguzi wa kidini.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam na Waandishi wa habari amesema hivi karibuni kanisa la Romani Katholic kupitia Umoja wao wa Maaskofu TEC tamko lao limekuwa likisambaa mitandaoni kuhusu sakata la bandari hivyo na kuzua taharuki miongoni mwa wananchi hivyo walichofanya waangalie kwani kila dini ikianza kuvalia njuga suala hilo linaweza kuleta shida hivyo wajifunze Miaka ya nyuma nchi ya Rwanda kilichotokea na mpaka Leo wanajutia ...

Sambamba na hayo amesisitiza kuwa Wananchi waangalie sana siyo kila kinachosambaa mitandaoni ni cha kukiamini vingine wavitazame na kuendelea na shughuli zao za kiuchumi kwani waangalie jinsi Rais Dkt Samia Suluhu Hassani anavyofanya kazi kuhakikisha maendeleo ya nchi yanasonga mbele hivyo wasitishwe na maneno ya kichochezi.

Ameongeza kuwa suala la maendeleo siyo suala la mtu binafsi bali  la jamii nzima ndiyo maana Rais Dkt Samia alitafuta wawekezaji kwenye sekta ya bandari ambapo badala yake baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wameanza kupotosha kuhusu uwekezaji huo kwa kuwahadaa watanzania.

Amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni amekuwa akipata vitisho kutoka kwa baadhi ya watu Mara baada ya yeye kuamua kukaa upande wa serikali kueleza mema yanayofanywa juu ya uwekezaji hasa wa bandari kwani watu hao wamekuwa wapinga maendeleo na wabinafsi

Hata hivyo amewasisitiza watanzania kuacha kufuata mkumbo kwani Rais Dkt Samia anapambana ili uchumi wa Tanzania uwe juu hivyo tusiyumbishwe na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wanaopinga maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages