HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 04, 2023

DK. SAMIA MGENI RASMI SIMBA DAY

 Na John Marwa


Klabu ya Simba imemtangaza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Simba Day 'Unyama Mwingi' siku ya jumapili Dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.




Simba wwanakwenda kuazimisha tamasha la 15 la Simba Day, likiwa limeanzishwa mwaka 2009. Limekuwa tamasha kubwa la michezo Barani Afrika ambalo huwakutanisha wanasimba na kuwatambulisha wachezaji wao.


Taarifa iliyotolewa asubui ya leo na klabu ya Simba kwenye mitandao ya kidijitali imeeleza kumkaribisha Rais Dkt Samia kwenye tukio hilo kubwa la michezo wikiendi hii.


"Karibu kwenye kilele cha wiki ya Simba. Karibu kwenye Simba Day, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hii ni siku muhimu kwa klabu ya Simba na wapenda michezo wote nchini Tanzania. 


"Tunakushukuru na tunakukaribisha kwa furaha kubwa isiyo kifani. Kwa kipekee kabisa, tunashukuru sana kwa mchango wako mkubwa kwenye sekta ya Michezo na Maendeleo Taifa kwa ujumla. Karibu Mheshimiwa Rais." Imeeleza taarifa hiyo.


Wakati Simba wakimtangaza namba moja wa nchi kuwa mgeni rasmi, tayari tiketi za tamasha hilo zilimalzika jana na kuweka rekodi ya kuuza tiketi siku mbili kabla ya siku ya tukio. 

No comments:

Post a Comment

Pages