Mkuu wa wilaya Mufindi, Dk. Linda Salekwa akikabidhi Kajuna Maurice zawadi ya bingwa wa mashindano ya gofu ya wazi ya Mufindi 2023
NA DENIS MLOWE, MUFINDI
MKUU
wa wilaya ya Mufindi Dr.Linda Salekwa ametoa pongezi kwa kampuni ya
Asas wazalishaji wa maziwa Bora nchini ya Asas kwa kudhamini mashindano
ya mchezo wa Gofu ya Mufindi Southern Open Championship 2023 na kushudia
Kajuna Maurice kutoka Lugalo gofu akiibuka bingwa wa mashindano hayo.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi zawadi kwa bingwa na washindi mbalimbali
wakiwemo wanawake na wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na kuendelea
, Dr. Salekwa alisema kuwa kampuni ya Asas imekuwa faraja kwa jamii ya
wanamichezo hivyo lazima waungwe mkono ili kuendelea kujitoa katika
kudhamini michezo mbalimbali nchini.
Licha
ya kuipongeza kampuni ya Asas alitoa wito kwa Wanawake wajitokeze kwa
wingi kushiriki michezo mbalimbali hususani mchezo wa Gofu kwa kuwa
katika dunia ya sasa michezo inatoa fursa ya ajira.
Alisema
kuwa mchezo wa Gofu ni ajira tosha hivyo yuko tayari kujifunza mchezo
huo wakati wowote na kuwaondoa hofu wanawake kwamba ni mchezo wa
gharama.
Aliongeza kuwa kiwanja Bora cha gofu
kiko kwenye wilaya ya Mufindi na serikali Iko tayari kuunga mkono mchezo
huo kwa kuwa ni Moja ya chanzo Cha mapato kwa wilaya kwa kuwa wageni
wengi wamekuja na kuingiza Hela maeneo haya.
Awali
akisoma risala ya mashindano hayo kwa mgeni rasmi, Mmoja ya washiriki
wa mashindano hayo , Yona Mbadime alisema kuwa mashindano yamekuwa na
mafanikio makubwa na kuweza kushirikisha wanamichezo takriban 44 ambapo
Wanawake walioshiriki ni 4 kutoka kwenye vilabu vitano vya Lugalo Gofu,
Kilombero , Gymkhana, Moshi na Mufindi.
Naye
mwakilishi kutoka kampuni ya Asas, Mohamed Salim ambaye ni afisa masoko
alisema kuwa kampuni hiyo Iko tayari kushirikiana na wanamichezo wa
mchezo huo na wasisite pindi wanapohitaji msaada
Alisema
kuwa mchezo huo unazidi kuwa kivutio kwani hauchagui rika katika
kucheza hivyo watu wajitokeze kushiriki na kufanya uwe na Wachezaji
wengi zaidi.
Katika mashindano hayo washindi walijinyakulia zawadi mbalimbali zikiwemo tv flat screen , friji na radio na fedha taslimu.
No comments:
Post a Comment