HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 24, 2023

KIJANI BOND 🌿 ya Benki ya CRDB ya kwanza Tanzania 🇹🇿, kubwa zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara

Benki ya CRDB leo imekabidhiwa kibali cha kuuza Hatifungani ya Kijani "Kijani Bond" ya miaka 5 yenye thamani ya dola za marekani 300 milioni sawa na Shilingi Bilioni 780 na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).


Kibali hicho cha kutoa hatifungani ya kijani kimekabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyeambatana na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Ally Laay katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.

Kibali hicho kinaifanya Benki ya CRDB kuwa ya kwanza nchini kutoa hatifungani ya kijani, na ya kwanza kwa ukubwa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kijani Bond itarahisisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kufadhili miradi rafiki kwa mazingira na kuchochea ufikiaji wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG).

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama (katikati), akikabidhi kibali cha kutoa hatifungani ya kijani "Green Bond" yenye ya thamani ya dola milioni 300 za Marekani sawa na Shilingi bilioni 780 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Ally Laay katika hafla iliyofanyika kwenye jijini Dar es Salaam jana. Hatifungani hiyo ni ya kwanza kutolewa Tanzania na ya kwanza kwa ukubwa Kusini mwa Jangwa la Sahaara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia), akizungumza katika hafla ya kupokea kibali kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) cha kutoa hatifungani ya kijani "Green Bond" yenye ya thamani ya dola milioni 300 za Marekani sawa na Shilingi bilioni 780. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Ally Laay na katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama.

Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama, akizungumza katika hafla hiyo.







 

No comments:

Post a Comment

Pages