HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2023

KIVUMBI NA JASHO SHIGONGO CUP TIMU 22 KUTOANA JASHO BUCHOSA.

TIMU 22 kutoka kata 21 za Jimbo la Buchosa  Wilayani Sengerema mkoani Mwanza zitachuana kusaka vipaji vya vijana wa Jimbo Hilo kutoka michuano ya Shigongo Cup mwaka 2023.

Michuano hiyo inaratibiwa na ofisi ya Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo imeanza kutimua vumbi julai 26 mwaka huu katika viwanja mbalimbali Jimboni humo.

Mbunge Shigongo  amegawa vifaa vya michezo kwa timu zote zitakazoshiriki mashindano hayo ambazo ni  jezi, mipira na 'track suit' vyenye thamani ya Tsh.million 16.
Shigongo amesema mashindano hayo yameanza kwa kushirikisha timu zilizoundwa kutoka Kila kata yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya vijana wa Jimbo Hilo.

"Buchosa inavija wengi wenye vipaji vya kucheza soka  hivyo tumeamua kuviibua na kuvionesha wa timu kubwa za simba,yanga,azamu na timu zingine za ligi kuu,ligi daraja la kwanza,daraja la pili na hata kuonekana  kwenda kucheza soka nje ya Tanzania"alisema Shigongo.

Mratibu wa Mashindano hayo Marco Zakalo amesema mashindano hayo yanahistoria ya kutoa wachezaji wengi kama khalfan Ngasa, Kenned Juma wa simba, sebusebu samsoni kipa wa geita gold na wachezaji wengine wengi waliopita katika mashindano hayo.

"viongozi waliopewa dhamana na kusimamia ligi hiyo wanatakiwa kuwa wazalendo kusimamia vyema mashindano ili kupata vipaji na washindi kwenye kata hizo"amesema Zagalo.
 
Diwani wa kata ya bupandwaMasumbuko Bupamba amesema kuanzishwa kwa ligi hiyo kutaitangaza vyema Buchosa  na kuibua vipaji ambavyo havijapata jukwaa la kuonekana huku akiwaomba vijana na mashabi wa soka kujitokeze kwa wingi kushangilia timu zao zinazoshiriki mashindano hayo.


No comments:

Post a Comment

Pages