HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2023

Waziri Dk. Pinda Chana atembelea Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Julai 31, 2023 Jijini Dar es Salaam ametembelea Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo amepitia hati ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara na Taasisi ya Elimu Tanzania.

Ushirikiano huo unalenga kuingiza maudhui ya harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika katika Mitaala ya kufundishia na kwenye vitabu vya kiada na ziada.

Mhe. Chana ameupongeza uongozi wa kituo hicho kwa jitihada za kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makubaliano hayo yanatarajia kusainiwa tarehe 7 Agost, 2023  Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Mawaziri wa pande zote mbili.


 

No comments:

Post a Comment

Pages