Na Mwandishi Wetu
UONGOZI wa Klabu ya Yanga unatarajia kuzindua Filamu 'Docomentary' maalumu kuhusu mapito ya mafanikio na changamoto ilizopitia katika Msimu wa 2022/23.
Uzinduzi huo unatarajia kufanyika Agosti 7, mwaka huu kwenye ukumbi wa Dar Free Market, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Ofisa habari wa Yanga Ally Kamwe amesema Docomentary hiyo maalumu, lengo ni kutunza kumbukumbu za Msimu wa kihistoria kwa vizazi vijazo.
"Filamu hii tumeshirikiana na wataalamu mbalimbali wa tasnia hii ya filamu na lengo kubwa ni kutunza kumbukumbu kwa kizazi kijacho kutokana na kile tulichokutana nacho.
Kamwe amesema ndani ya Filamu hiyo pia wataonesha kila kitu katika safari zao za ndani na nje ya nchi, changamoto walizopitia kuelekea mafanikio hayo.
Ameongeza kubwa kwa Tanzania, Yanga ndio timu ya kwanza kuandaa filamu hiyo na watakuwa chini ya udhamini wa Benki ya NMB ambayo wamekuwa nayo bega kwa bega.
Kwaupande wake Haji Mfikirwa ambaye ni Mkurugenzi wa Wanachama amesema wameandaa utaratibu maalumu kwa ajili ya kuwaalika watu katika uzinduzi huo.
"Tunatarajia kutoa mualiko kwa makundi mbalimbali na mwaliko huo tutakuwa tunataarifiana taratibu unajua Yanga inawatu wengi wa kada mbalimbali tumezingatia hilo," amesema Mfikirwa.
Amesema uandaaji wa filamu hiyo unaonesha namna uongozi wao ulivyokuwa makini na kuumiza kichwa katika kufikiria namna ya kuwapa raha watu wake.
No comments:
Post a Comment