HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 03, 2023

MFALME NDANI YA MBUGA YA WAFALME

Na John Marwa


Mfalme wa muziki Tanzania Ali Kiba 'KingKiba'. Amejiunga na timu bora ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Simba SC na rasmi kutumbuiza kilele cha Simba Day Unyama Mwingi' katika Dimba la Benjamin Mkapa Agosti 6.


Tukio la kutambulishwa kwa Ali Kiba 'KingKiba' limefanyika usiku huu jijini Dar es Salaam na   Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Imani Kajula.


Ali Kiba 'KingKiba' baada ya kutambulishwa kutoa kwenye kibegi pati 3, amesema amepata mapokezi makubwa kutoka kwa Wanasimba  na Moyo unapenda unapo thaminika.


"Nimepata mapokezi makubwa Simba, moyo unapenda unapo thaminika. Kiukweli nilikuwa nawaonea wivu saaa Wanasimba. Asanteni kwa kunikaribisha." Amesema KingKiba.


Hata hivyo kwa upande wa klabu ya Simba imeeleza kuwa .


"Rasmi Staa wa Muziki wa Tanzania na Afrika, Ally Kiba 'King Kiba' amehamia kwetu na Simba Day Agosti 6 atakuwa mtumbuizaji mkuu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.


Baada ya kutambulishwa Ali Kiba ametambulishwa wimbo mpya wa Klabu ya Simba unaoitwa MNYAMA na umepokelwa kwa kishindo na mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages