HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 05, 2023

SABABU ZA RAIS DK. SAMIA KUWA MGENI RASMI SIMBA DAY

NA JOHN MARWA


SIKU moja baada ya Uongozi wa klabu ya Simba kumtangaza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi, ni kwa sababu ya ukubwa wa timu hiyo kuelekea siku kubwa ya tamasha lao katika kilele cha siku Simba Day.



Ikiwa ni Simba Day ya Unyama Mwingi makala ya 15, Simba watakutana Dimba la Benjamin Mkapa, Temeke jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata burudani mbalimbali na kuwatambulisha Wanajeshi wao watakaowaongoza kwenye vita ya msimu mpya wa Mashindano mbalimbali.


Tamasha la Simba Day litakalofanyika kesho (Jumapili) na Simba watatumia kutambulisha wachezaji wao wa msimu 2023/24 pamoja na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Power Dynamos ya Zimbia, ambao waliwasili nchini jana jioni.


Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amaiambia Habari Mseto kuwa Simba Day ya mwaka huu ni kubwa na maalum na sikukuu, hali iliyopelekea kumuomba Rais Dk. Samia kuwa mgeni rasmi. 


Amesema uongozi wa Simba unamshukuru Dk Samia kukubali mwaliko wao na kuwa miongoni mwa watanzania 60,000, watakao hudhuria Simba Day mwaka huu ambayo itakuwa ya aina yake.


“Maandalizi ya Tamasha hili la historia yanaendelea vizuri,  kila kiti kipo kwenye mstari  huku taratibu zikiwa vizuri na kusubiriwa siku yenyewe kufika ili mashabiki kupata burudani siku hiyo kuanzia wasanii na mechi mbalimbali za kirafiki ambazo zitacheza na timu zote za Simba.


"Simba inatimu ya wanawake, vijana na kubwa zote zitapata utambulisho, kubwa zaidi itatumika kumtambulisha kipa wetu mpya badala ya Mbrazil Jefferson Luis ambaye ni majeruhi,” amesema Ahmed.


Ameongeza kuwa kuna mambo makubwa ambayo wanatarajia kuyafanya ndani ya siku hiyo, tayari tiketi za tamasha zimeuzwa zote,  ni wazi mashabiki 60,000 wamethibitisha kuhudhuria Simba Day 2023 ikiwa ni historia mpya kwa kuwa haijawahi kutokea.

No comments:

Post a Comment

Pages