HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 05, 2023

ZANZIBAR HOI CECAFA U-18

TImu ya Zanzibar ya Wanawake U-18 imemaliza Mashindano ya Wasichana U18 ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA bila ya ushindi.



Mchezo wa mwisho kwa Zanzibar umemalizika kwa Zanzibar kupoteza kwa mabao (4-0) dhidi ya Burundi.


Matokeo hayo yameifanya Zanzibar kushika nafasi ya mwisho kati ya Mataifa matano yaliyoshiriki Mashindano hayo.



Wakati Burundi wao ni ushindi wao wa kwanza kati ya michezo minne waliyoicheza, huku wakipoteza mechi tatu za awali dhidi ya Uganda, Tanzania na Ethiopia.


Kipindi cha kwanza timu zote zilianza kwa kasi ya kushambuliana, dakika ya pili Burundi walikosa nafasi ya wazi baada ya mabeki wa Zanzibar kushindwa kuondosha mpira ndani ya boksi.


Dakika mbili mbele walirejea makosa yaleyale na Rukiya Bizimana dakika ya 4 akapachika bao la kuongoza kwa mkwaju mkali uliomshida mlinda lango. 


Zanzibar walirejea mchezo baada ya kuruhusu bao hilo kwa kucheza kandanda safi ya pasi fupi fupi huku have wakishindwa kutumia nafasi kadhaa walizozitengeneza.


Dakika ya 45 ilipigwa krosi langoni mwa Zanzibar na iliyomshinda mlinda lango huku Wiggo Magoma akijifinga katika harakati za kuokoa.



Kipindi cha pili Burundi walirejea kwa kuchukua mchezo jambo lililopelekea kuandika bao la tatu dakika ya 48 kupitia kwa kiungo mshambuliaji Adolphine Rumuri akitumia makosa ya mlinda lango wa Zanzibar kuutokea mpira.


Dakika ya 69 Adolphine Rumuri alipiga msumari wa nne kwa Burundi na kuhitimisha karamu ya ushindi huo na kuwaachia simanzi Zanzibar.



Kikosi cha msimu Zanzibar, langoni Aisha Said, Wiggo Magoma, Rahma Nassor, Jacqueline Solomoni, Rukia Laizer, Agnes Millanzi, Mwamvita Muba, Hawa Juma,  Saada Said, Zainab Nassad na Fatma Bakari.


Kikosi cha Burundi langoni Amissa Inakurundo, Chanceline Akimana, Evelyne Akimana, Neema Nzohabonayo, Estella Gakima, Channy Nsabiyumva, Bora Ineza, Rukiya Bizimana, Yasinta Marimba, Adolphine Rumuri na Zena Nahimana.

No comments:

Post a Comment

Pages