Na John Marwa
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU imefungua Dirisha la pili ni udahili Leo, baada ya dirisha la kwanza kufungwa leo Agosti 25, 2023.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Charles Kihampa amesena awamu ya kwanza imekamilika leo na dirisha la pili limefnguliwa.
"Leo Agosti 25, 2023, Dirisha la udahili wa awamu ya kwanza umekamilika, katika awamu hii ya kwanza tulikuwa na jumla ya waombaji 116,133 hawa ndio walifanikiwa kutuma moombi yao moja kwa moja kwa Vyuo 80 vya Elimu ya Juu ambavyo vilikuwa vimeruhusiwa kudahili wanafunzi kwa Shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2023.
"Katika hivyo Vyuo 80 tulikuwa na jumla ya programu 809, hii ukilinganisha na mwaka jana tulikuwa na programu 757 tuna jumla ya programu 52 za masomo ambazo zimeongezeka, kuongezeka kwa hizo programu pia kumeongeza nafasi zaidi, kwaiyo mwaka huu tuna nafasi 186, 289, hili ni ongezeko la asilimia 8.2, kwaiyo tunazo hizo nafasi kwa Shahada ya kwanza kwa Vyuo vya elimu ya juu."amesema Kihampa na kuongeza kuwa.
"Mpaka sasa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza tuna waombaji 86,624, kati ya wale 116, 133 hawa wameshapata nafasi, waombaji 86,624 sawa na asilimia 74.6 hawa wameshapata nafasi kwenye Vyuo ambavyo walituma maombi yao kuomba kudahiliwa kwa Shahada mbalimbali, kwa Shahada ya kwanza katika programu mbalimbali.
"Kwa sababu kila mwanafunzi alituma maombi yake kwenye Chuo anachokipenda, kuna kuwa na wale ambao wanaweza kuwa wamepata udahili zaidi ya chuo kimoja, sasa hawa waliopata udahili zaidi ya Chuo kimoja watapokea ujumbe mfupi na namba ya siri pia namba za simu ambazo walizitumia wakati wanaomba udahili lakini pia kupitia barua pepe zile ambazo waliziweka wakati wanafanya udahili.
"Lakini ikitokea kuwa hajapa ujumbe mfupi anatakiwa kuingia katika mfumo wa Chuo chochote ambacho amepata udahili, kuna mahali ataona ataomba kutumiwa ujumbe mfupi ili aweze sasa kujithibitisha kwenye chuo kimoja wapo ambacho anakipenda.
"Zoezi hili la kuthibitisha kwenye chuo ambacho mwanafunzi anakipenda kwa wale walioomba na kupata udahili zaidi ya chuo kimoja linaanza leo Agosti 25 hadi Septemba 9, 2023. Kwaiyo nitoe wito kwa wanafunzi wote waliopata zaidi ya Chuo kimoja, watumie ule ujumbe mfupi kuweza kujithibitisha."amesema.
Amebainisha kuwa majina ya wale waliopata zaidi ya Chuo kimoja yanapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu TCU, hivyo waingie kwenye hiyo tovuti wataona Vyuo walivyopata katika tangazo hilo.
"Tume inatangaza kwamba Dirisha la pili la udahili wa Shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2023/24 limefunguliwa rasmi leo Agosti 25, 2023 na litakaa kwa takribani siku 12 mpaka Septemba 6, 2023.
"Nitoe wito hapa kwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi katika ile awamu ya kwanza au wale ambao hawakufanikiwa kupata Vyuo katika ile awamu ya kwanza basi watumie fursa hii vizuri ili kuweza kutuma maombi moja kwa moja kwenye Vyuo wanavyovipenda." ameongeza kuwa.
Nitoe wito pia kwa Vyuo vyetu vya elimu ya juu ambavyo vina dahili wanafunzi kwa mwaka huu wa masomo 2023/24, wafungue zile programu ambazo zina nafasi, ikumbukwe kwamba baadhi ya programu zinaweza kuwa zimejaa Sasa wafungue zile programu ambazo zina nafasi."amesema Kihampa."amesema.
Hata hivyo amesema kuwa majina ya wale waliopata Vyuo yanatangazwa na Vyuo vyenyewe kwa wote wale ambao walifanya dahili katika dirisha la kwanza.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa,
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 25,
2023 wakati akitangaza kukamilika kwa Awamu ya Kwanza na kufunguliwa kwa
Awamu ya Pili ya Udahili wa Shahada ya Kwanza kwa Mwaka wa Masomo 2023/
2024.


No comments:
Post a Comment