HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 01, 2023

SHIUMA WAMFUKUZA NAIBU KATIBU MKUU WAO

Katibu Mkuu wa Shiuma Taifa - Venatus Magayane akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa shiuma taifa Matondo Masanja akizungumza na wamachinga wilaya ya Iringa Mjini.
 Mgeni rasmi Katika mkutano huo Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Michael Semindu akitoa neno.

Baadhi ya viongozi wa muda wa Shiuma wilaya ya Iringa wakikabidhiwa katiba ya Shiuma.

 
 
 

NA DENIS MLOWE, IRINGA
 

Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini (SHIUMA) kupitia katika mkutano uliofanyika mkoani Iringa wa kuchagua viongozi wa masoko mkoani hapa wamemfukuza aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa shirikisho Hilo Joseph Mwanakijiji kutojihusisha na shirikisho Hilo nchini.
 

Maamuzi hayo yametolewa na uongozi wa shirikisho Hilo wakati wa uchaguzi wa viongozi wa muda wa shirikisho Hilo kwa wilaya ya Iringa uliofanyika katika soko la Mwamwindi Mlandege.
 

Akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu wa SHIUMA Taifa, Venatus Magayane alisema Kamati Kuu ya SHIUMA iliyokutana hivi karibuni imejiridhisha pasipo shaka kwamba Joseph Mwanakijiji anakosa sifa za kuendelea kuwa Naibu Katibu Mkuu wa SHIUMA nchini na kutaka kutojihusisha na shirika Hilo nchini.


Alisema akiwa Naibu Katibu Mkuu ,Mwanakijiji alishindwa kufanya kazi yake ipasavyo na uongozi ulipofika hapa kuuliza kuhusu shiuma kwa wamachinga walikuwa hawalitambui hivyo ameshindwa kuinadi SHIUMA na Katiba yake kwa machinga wa Iringa pamoja na kwamba kwa kupitia shirikisho hilo amekwenda mikoa mbalimbali nchini kulitangaza shirikisho hilo.


Aidha Alisema kuwa chanzo kingine ni migogoro ya mara kwa mara ya wamachinga wilaya ya Iringa ambapo baada ya kufuatilia migogoro na vurugu za mara kwa mara zilizokuwa zikifanywa na machinga wa Iringa alisema wamebaini kiongozi huyo alikuwa sehemu yake kinyume na katiba ya Shiuma.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanja aliwataka viongozi wa muda wa Shiuma wilaya kuwaunganisha na kuwasajili machinga katika shirikisho hilo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa viongozi wake.

Masanja alitoa onyo kwa uongozi huo akisema atakayebainika kuhamasisha vurugu,maandamano na migomo inayohatarisha amani na usalama wa mali na raia wengine atachukuliwa hatua za kisheria na kutoa wito kwa jeshi la Polisi kushughulika nao.


"Lengo la shirikisho ni kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ya wamachinga nchini hivyo yoyote atakayeanzisha migogoro isiyo na tija atakuwa Hana nafasi kwenye shirikisho Hilo na ikitokea changamoto basi Kuna umuhimu wa kukaa meza Moja kuliko kuanzisha migogoro isiyo na tija.

Alisema kuwa SHIUMA ni chombo kinachofanya kazi na serikali katika kuwaendeleza machinga na biashara zao. Jambo lolote linaloleta tofauti baina ya pande hizo mbili litamalizwa kupitia meza ya majadiliano na sio kwa kuhamasisha vurugu au maandamano ama maandamano.


Naye mgeni rasmi Katika mkutano huo Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Michael Semindu alisema kuwa serikali imeahidi kuwapa ushirikiano mkubwa wamachinga nchini wakati wowote

Alisema kuwa Serikali Iko na wamachinga popote hapa nchini na kutoa ushirikiano na kukaa kwenye meza ya mazungumzo kwenye changamoto yoyote inayojitokeza


Alisema kuwa wilaya ya Iringa imeandaa idara ndogo ya serikali ambayo itafanya kazi Kwa karibu machinga ya kufanya kazi pamoja kuondoa changamoto za machinga zilizopo pindi zinapojitokeza.


Akizungumzia ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania aliyotoa milioni 10 ya kujenga ofisi ya wamachanga alisema kuwa wanatarajia kujenga ofisi ya kisasa na ya mfano ambayo itakuwa na kumbi ya mikutano na ofisi mbalimbali ikiwemo ofisi ya afisa biashara kwa Lengo la kuiweka pamoja na wamachinga kutatua kero zao.


No comments:

Post a Comment

Pages