Na Magrethy Katengu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewashauri wakazi wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa zitakazotokana na mkutano wa Jukwaa la mfumo wa chakula la Afrika (AGRF), kwa lengo la kuongeza ujuzi, uzoefu na kujifunza teknolojia za kisasa katika sekta ya Mifugo na Kilimo ili kutimiza malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kulisha Dunia.
Chalamila ameyasema leo Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF), unaotarajia kuanza tarehe 5-8 Mwezi huu katika Kituo Cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Jijini humo.
“Mkutano huu utaleta matokeo muhimu katika uendelezwaji wa mifumo ya chakula Afrika , ukuzaji wa sekta ya Utalii, Biashara na Uwekezaji, na kukuza teknolojia mpya” amesema Chalamila.
Naye, Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Ephrahim Mafuru, amesema Serikali inatatarajia kupokea wageni zaidi 3000 wa masuala ya kilimo, na ambapo jumla ya sh. Bilioni 12.5 zimetolewa kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo kuanzia maandalizi hadi kuhitimisha Mkutano huo
“Mchango wa kituo katika mnyororo wa thamani hivyo Serikali kwa kushirikiana na AGRF imejipanga kwa bajeti ya Bilioni 12.500 na fedha hizo ni maandalizi ya mkutano ambazo zitaingia katika mnyororo wa thamani wa maandalizi na gharama za kuuendesha mkutano huo,”amesema.
Jukwaa la mfumo wa chakula la Afrika (AGRF) ni jukwaa kuu la kilimo linalowakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo ili kujadili na kuchukua hatua za kiutendaji katika kuboresha njia za upatikanaji na usalama wa chakula na lishe kwa ujumla.
Aidha amewataka wakazi hao kudumisha usalama, ukarimu na usafiri ili kuweka taswira nzuri kwa wageni watakaofika.katika mahoteli ya Jiji la Dar es Salaam na wananchi kwa ujumla kutumia fursa zitakazopatikana katika mkutano huo ili kuboresha shughuli za kilimo na Ufugaji.
September 02, 2023
Home
Unlabelled
WATANZANIA CHANGAMKIENI FURSA ZA. MKUTANO WA AGRF
WATANZANIA CHANGAMKIENI FURSA ZA. MKUTANO WA AGRF
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment