Kamanda
wa Polisi mkoa wa Songwe ACP Theopista Mallya, amewataka waamini wa
kanisa la T.A.G Bethlehem Revival Temple kuendelea kufanya matendo mema
na kukemea matendo maovu wanapokuwa kanisani mpaka kwenye himaya zao ili
kupunguza vitendo viovu katika jamii.
Kamanda
Mallya ameyasema hayo Oktoba 14, 2023 wakati akitoa elimu ya
Ushirikishwaji wa Jamii katika Mkutano wa Injili ulioandaliwa na kanisa
hilo eneo la Mlowo wilaya ya Mbozi.
“Tumshike
Mungu waamini wenzangu na kuyatenda yale yote aliyoyaelekeza katika
biblia takatifu pia kuyaishi ili kutokomeza vitendo viovu katika jamii
zetu na kwa umoja wetu tusijihusishe na vitendo vya uhalifu na ukatili
ikiwa ni pamoja na unyanyasaji kwa watoto” Alisema Kamanda Mallya.
Kamanda
Mallya aliendelea kuwasihi waamini wa kanisa hilo walioudhuria katika
mkutano huo wa Injili kuacha ulevi uliopindukia na kutoamini imani
gombanishi za kishirikina kwani kufanya hivyo kutapunguza vitendo vya
ukatili wa kijinsia na unyanyasaji katika mkoa wetu.
Kwa
upande wa waamini wa kanisa hilo wamepongeza elimu iliyotolewa na
kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment