Waziri
wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameutaka Mgodi wa Singida Gold Mine
unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Mine kuharakisha ulipaji wa fidia kwa
wananchi waliopo ndani ya eneo la leseni ambao walikuwa bado
hawajalipwa.
Amesema hayo leo Oktoba 14, 2023 alipotembelea Mgodi huo wilayani Ikungi mkoani Singida kujionea maendeleo ya mradi huo.
Waziri
Mavunde amesema kuwa mgodi huo umefanya kazi kubwa ya kuhakikisha
wanatimiza masharti ya leseni ya uchimbaji hivyo ni muhimu kuharakisha
ulipaji wa fidia kwa wananchi waliokuwa bado hawajalipwa.
“Niwapongeze
kwa hatua mliyopiga ndani ya kipindi kifupi, niwahimize kuharakisha
suala la fidia kwa wananchi ambao bado, hii itawasaidia nyie kufanya
shughuli zenu bila malalamiko ya wananchi wa maeneo yanayowazunguka, na
kwa kuwa wamebaki wachache naamini halitachukua muda mrefu sana" amesema
Mavunde.
Pia, Mhe. Mavunde ameuhimiza Mgodi wa Singida
kuendelea kuboresha mahusiano mazuri na wananchi wanaozunguka mgodi huo
kwa kuendelea kuwaboreshea miundombinu yao kupitia Wajibu wa Kampuni kwa
Jamii (CSR) pamoja na kuwapa kipaombele wazawa katika utoaji wa huduma
katika mgodini kama sheria inavyotaka.
Kwa upande wake, Meneja
Mkuu wa Singida Gold Mine, George Kondela amesema kuwa tayari Mgodi
umewalipa fidia ya ardhi wananchi 236 na kuwajengea nyumba wananchi 12,
na kwamba wanashughulikia fidia ya ardhi kwa wananchi 53 waliosalia na
nyumba za wananchi 10.
Aidha, ameongoza kuwa mgodi huo
unaendeshwa na wazawa kwa asilimia 100 kwa hatua zote kuanzia kwenye
usanifu, ujenzi na uendeshaji.
October 15, 2023
Home
Unlabelled
WAZIRI MAVUNDE AUTAKA MGODI WA SINGIDA GOLD KUHARAKISHA FIDIA KWA WANANCHI
WAZIRI MAVUNDE AUTAKA MGODI WA SINGIDA GOLD KUHARAKISHA FIDIA KWA WANANCHI
Share This

About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment