NA TULLO CHAMBO, RT
BAADA ya kuzinduliwa na kutambuliwa rasmi, Kamati Maalumu ya Marekebisho ya Katiba ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), imeweka hadharani namna ya kupokea maoni ya wadau ili kufanikisha zoezi hilo muhimu kwa mustakabali wa mchezo huo.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Katibu wa Kamati hiyo, Wilhelm Gidabuday, imewahimiza wadau kujitokeza kushiriki zoezi hilo, kwani maoni na mapendekezo yatafanywa na wao na kazi ya Kamati itakuwa kuyaweka katika mfumo wa rasimu, kabla ya kuwasilishwa Kamati Tendaji RT na kisha Mkutano Mkuu kwa ajili ya kupitishwa.
Kamati hiyo, imeweka wazi utaratibu huo kama ifuatavyo:
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.
01.12. 2023.
Arusha.
1. Kamati ya Marekebisho ya katiba iliyoundwa na Shirikisho la Riadha Tanzania na kuanza kutekeleza majukumu ya kazi hiyo tarehe 16.10.2023, imeendelea na mchakato wa shughuli zake kwa kupitia nyaraka mbalimbali ili kuisadia kutimiza wajibu huo kikamilifu.
2. Kamati inapenda kuwatangazia kuwa mchakato wa marekebisho ya katiba utafanywa na wadau na wakereketwa wa mchezo wa riadha wenyewe na kazi ya kamati ni kuyaratibu maoni hayo na kuyaunganisha kwa kuyatafsri katika muundo wa rasimu ya Katiba itakayowasilishwa kwa kamati ya utendaji ya shirikisho la riadha Tanzania (RT) na baadaye mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho kwa ajili ya maamuzi.
3. Kwa mazingatio hayo, kamati inawatangazia rasmi kuwa maoni hayo yatawasilishwa na kukusanywa mbele ya kamati kwa kupitia mfumo/utaratibu wa njia kuu mbili (2).
3.1. Kujaza dodoso maalum ambalo litapatikana kwa kila katibu mkuu wa chama cha riadha cha mkoa mwanachama wa shirikisho. Ukisha jaza dodoso hiyo utairejesha kwa katibu wa mkoa wako husika au waweza kuiwasilisha kwa mjumbe wa kamati aliye karibu na mahali ulipo au kuituma mwenyewe kwenye akaunti ya kamati rekebishakatiba@gmail.com moja kwa moja.
3.2. Kujaza dodoso la kimtandao (google docs) kupitia rink maalum ya maswali https://forms.gle/fgcwhQhPvLkX38xo7– ukishajaza itakweleza kuwasilisha (submit).
4. Kamati inapenda kusisitiza kwamba, maoni hayo yakishakusanywa na kuratibiwa ndiyo yatakayotengeneza rasimu mpya ya katiba ya shirikisho, hivyo kila mdau na mkereketwa wa mchezo huu anao wajibu wa kutumia fursa hii muhimu kupitia mfumo na utaratibu uliowekwa.
5. Kamati inawatangazia wadau wote kwamba dirisha la kukusanya maoni litakuwa la siku 35 (thelathini na tano) kuanzia siku na tarehe ya tangazo hili.
Karibuni – kwa maendeleo ya riadha nchini na ustawi wa kiuchumi wa Taifa letu.
Kamati inawatakiwa sikukuu njema ya Christimas 2023 na heri ya mwaka mpya 2024.
Imetolewa na katibu wa kamati.
Wilhem F. Giddabuday
SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA
‘Kamati ya ukusanyaji maoni na mchakato wa marekebisho ya katiba ya Shirikisho’
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.
01.12. 2023.
Dar es salaam.
MAKUNDI MAALUM YANAYOKUSUDIWA.
S/NA |
KUNDI |
IDADI |
MRATIBU |
1 |
Kamati ya Utendaji iliyopo madarakani |
15 |
|
2 |
Wenyeviti wa Mikoa – Mkoa Mwanachama |
30 |
|
3 |
Makatibu wa Mikoa |
30 |
|
4 |
Baraza la Michezo la Taifa |
10 |
|
5 |
Viongozi wa kisiasa |
15 |
|
6 |
Viongozi wastaafu - RT |
10 |
|
7 |
Kamisheni ya wachezaji |
25 |
|
8 |
Wanariadha wakongwe |
15 |
|
9 |
Wanariadha wa kimataifa wanaocheza sasa |
15 |
|
10 |
Wanariadha wa kitaifa |
30 |
|
11 |
Wakereketwa wa riadha nchini |
15 |
|
12 |
Wana taaluma wa taaluma ya michezo · Vyuo vya kati · Vyuo vikuu |
20 |
|
13 |
Kundi mchanganyiko |
40 |
|
14 |
Uwakilishi wajumbe wa kamati tendaji za mikoa |
60 |
|
15 |
Wana Habari wakereketwa na mchezo wa riadha |
20 |
|
|
Jumla |
350 |
|
No comments:
Post a Comment