NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mamlaka
ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani katika kuanza wiki ya shukrani
kwa mlipa kodi imeamua kurudisha fadhila kwa jamii kwa kutoa msaada wa
vifaa mbali mbali vya ujenzi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa jengo la
mama na mtoto lililopo katika zahanati ya Misugusugu halmashauri ya mji
Kibaha.
Akizungumza katika halfa ya kukabidhi msaaada wa vifaa hivyo Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Masawa Masatu alisema kwamba wameamua kusapoti sekta ya afya kwa lengo la kuweza kuwakomboa wakinamama kupata huduma bora hasa wakati wa kujifungua.
Meneja
huyo alibainisha kwamba TRA katika zahanati ya misugusugu kuna
changamoto ya miundombinu ya jengo la mama na mtoto hivyo wakaona kuna
umuhimu wakusaidia vifaa hivyo ambavyo vitasaidia katika ujenzi huo.
"Tupo
katika wiki ya shukrani kwa mlipa kodi na sisi kama TRA Mkoa wa Pwani
tumeona ni vuzuri tukaungana na wananchi katika ujenzi huu ambao
utasaidia kwa kiasi kikubwa changamoto ya wakinama kupoteza maisha yao
hasa wakati wa kujifungua,"alisema Masatu.
Meneja
alisema kuwa ana imani msaada huo utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa
wanawake wa kata ya misugusugu na maeneo mengine kuweza kupata fursa ya
kuweza kuondokana na usumbufu waliokuwa wanaupata katika kipindi cha
nyuma.
Kwa
upande wake Afisa Maendeleo ya jamii wa kata hiyo, Kezia Olambo
aliwashukuru kwa dhati TRA kwa msaada huo wa kuisaidia jamii katika
suala zima la kuboresha sekta ya afya.
Alisema
wananchi wa kata hiyo wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu
kwenda kutafuta huduma za mama kujifungua katika eneo la Mlandizi na
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Pwani ya Tumbi jambo ambalo limekuwa
likichangia kuongea Vifo vya mama na mtoto.
"TRA
tunawashukuru Kwa kutupatia msaada wa vifaa hivi vya ujenzi maana
ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati hii itaokoa maisha ya
wanawake wanahitaji huduma ya kujifungua maana wengi wamekuwa wakitoka
hapa kwenda kufuata huduma mlandizi au hosptali ya rufaa ya mkoa wa
Pwani"alisema
Naye
Afisa mtendi wa kata hiyo, Elizabeth Mwakalikwa, alisema ujenzi wa
jengo Hilo utagaharimu zaidi ya shilingi milioni 60, na kwamba bado
jitihada za makusudi zinahitajika ili kumalizia ujenzi huo na kuwaomba
wadau wengine kujitokeza ili kukamilisha mradi huo.
"TRA
wametupatia msaada na tunamshukuru na kupitia msaada huu tutaendelea
kuhamasisha wananchi kulipa Kodi Kwa ajili ya maendeleo yetu
wenye...ujenzi huu bado haijakamilika tunaomba wadau wengine wajitokeze
kutoa misaada ambayo itusaidia"alisema
Swaiba
Kaisi mkazi wa kata ya misugusu, alisema kukamilika Kwa ujenzi wa jengo
Hilo litakuwa mkombo Kwa wanawake kuondokana na adhamba ya kutembea
umbali mrefu kufuata huduma umbali mrefu ambapo utapunguza vifo vya
wanawake wajawazito.
Katika
hatua nyingine mamlaka hiyo imetoa msaada wa vyakuka na vinywaji katika
kituo Cha watoto yatima cha Fadhillah Ophanage Center ambayo ni,
sabuni, unga, Mchele, mafuta, sukari na mahitaji mengi ya msingi.
Kauli
mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ya mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa
Pwani katika wiki ya shukrani kwa mlipa kodi inasema kodi yetu
maendeleo yetu tuwajibike.
No comments:
Post a Comment