NA MWANDISHI WETU
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele ambaye kwasasa anakipiga Pyramids ya Misri ameingia tatu bora katika tuzo ya mchezaji wa mashindano ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF akiburuzana na staa wa Al Ahly, Percy Tau na Petter Shalulile anayekiwasha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Tuzo hizo zitatolewa Desemba 11 nchini Morocco.
Kama Mayele atafanikiwa kutwa tuzo hiyo itakuwa Tuzo ya pili kuchukuliwa na mchezaji kutoka klabu ya Tanzania kwa maana ya mafanikio ambayo aliyapata alikuwa akiitumikia Yanga SC.
Pape Osmane Sakho aliwahi kutwa tuzo ya Bao bora la msimu akiwa na jezi ya Mnyama Simba ambapo alifanikiwa kuifikisha Simba hataua ya Robo Fainali ya Kombela Shirikisho CAF CC katika msimu huo.
Bao hilo alilifunga katika mchezo wa hatua ya makaundi dhidi ya Asec Mimosas. Wakati Mayele msimu uiopita aliifikisha Yanga Faianli ya CAF CC akiibuka kinara wa mabao saba.
No comments:
Post a Comment