Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (kushoto) akizungumza na Rais wa Benki ya Dunia, Ajaypal Singh Banga. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa NMB,Vicky Bishubo na Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna ameshiriki uzinduzi wa
Mkutano Mkuu wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review) unaofanyika kwa
siku tatu Zanzibar.
Mkutano huo umefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi - Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi na kuhudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar - Hemed Suleiman Abdalla, Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Mhe. Mwigulu Nchemba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania - Emmanuel Tutuba na viongozi wengine.
Benki ya NMB inajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha mkutano huu mkubwa Tanzania unao wakutanisha wajumbe zaidi ya 3,000 kutoka mataifa takribani 100 duniani.
No comments:
Post a Comment