Afisa Mwandaamizi wa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Sabato Kosuri akifungua Kikao kazi baina OSHA na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na OTR na kufanyika Jijini Dar es Salaam Disemba 7, 2023.Baadhi ya Wahariri na Waandishi wa habari wakiwa kwenye Kikao kazi hicho.
Na Mwandishi Wetu
Katika
kipindi hiki cha Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu
Hassan, Tanzania imeweza kupaa hadi kutambuliwa na Mashirika ya
Kimataifa na nchi mbalimbali duniani kama nchi yenye mifumo bora ya
usimamizi wa masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi.
Ubora huo
wa mifumo umetazamwa katika maeneo muhimu mamtatu ambayo ni Uwepo wa
chombo mahsusi cha kusimamia masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi
ambacho ni Taasisi ya OSHA, Uwepo Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia
masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi na Uwepo wa mifumo ya
usimamizi wa masuala ya Usalama na Afya katika ngazi ya maeneo ya kazi
(at enterprise level).
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda, alipokuwa
akitoa Taarifa ya Utendaji na mafanikio ya OSHA ndani ya miaka mitatu ya
Uongozi wa Rais Dk. Samia, wakati wa Kikao kazi baina yake (Khadija) na
Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR)
na kufanyika Jijini Dar es Salaam Disemba 7, 2023.
Alifafanua
kuwa uwepo wa nyenzo (maeneo hayo matatu yaliyotajwa unaendana na
matakwa ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) jambo ambalo limewezesha nchi
mbalimbali Barani Afrika kama Kenye, Zimbabwe na Lesotho kuja kujifunza
juu ya mifumo iliyopo Tanzania.
Khadija alisema, kutokana na
Tanzania kuaminika, Msimamizi wa Dawati la Usalama na Afya kwa nchi za
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ni mtumishi kutoka
OSHA, hiyo ikiwa ni kutokana na uongozi bora wa Serikali ya Awamu ya
Sita, ambayo imeona umuhimu waTaasisi hiyo na kuipandisha hadhi kwa
kuiwezesha kusimamia masuala ya Usalama na Afya kwa kuipatia wataalam,
vitendea kazi na rasilimali nyinginezo muhimu katika kufanikisha
utekelezaji wa malengo yaTaasisi hiyo.
Alisema, katika kipindi
hiki cha miaka hiyo mitatu ya Rais Dk. Samia, Taasisiya OSHA imepata
mafanikio makubwa ambayo yametokana na kuendana na utekelezajiwa Ilani
ya Chama Tawala (Chama Cha Mapinduzi-CCM), Ibara ya 130 (f) ambapo Chama
kimewaahidi Watanzania kwamba kitajenga uwezo wa waajiri na wafanyakazi
kuhusu afya na usalama mahali pa kazi.
Akieleza mafanikio
Mtendaji Mkuu huyo alisema, kwa kipindi cha miaka hiyo mitatu ya uongozi
wa Rais Dk. Samia OSHA wamepata mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza
maoneo ya kazi yaliyosajiliwa hadi kufikia 30,309 na pia kwa miaka hiyo
mitatu wameweza kuimarisha shughuli za usimamizi wa usalama na afya
mahali pa kazi nchini.
“Katika kipindi tajwa, wakala umefanikiwa
kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa kutoka 4,336 hadi
30,309, ongezeko hili ni sawa na asimilia 599. Aidha idadi ya kaguzi
zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia kaguzi
776,968 sawa na asilimia 646,”alisema.
Alisema kaguzi hizo
zinahusisha, ukaguzi wa jumla, ukaguzi maalum kama vile ukaguzi wa
usalama wa umeme, Vyombo vya Kanieneo, ukaguzi wa vifaa vya kunyanyulia
vitu vizito, ukaguzi wa kiegonomia pamoja na tathmini ya vihatarishi vya
kimazingira.
Alitamba zaidi kwamba kumekuwa na ongezeko la
asilimia 44.1 ya wafanyakazi waliopata mafunzo ya usalama na afya mahali
pa kazi kutoka wafanyakazi 32,670 hadi kufikia 47,090 akifafanua kuwa
mafunzo hayo yanajumuisha ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya
mahali pa kazi na uundwaji wa Kamati za Usalama na Afya, mafunzo ya
kufanya kazi katika maeneo ya juu, Huduma ya Kwanza, Usimamizi na
Udhibiti wa Kemikali katika maeneo ya kazi, Usalama na Afya katika sekta
za Mafuta na Gesi na sekta ya Ujenzi na Majenzi na Uendeshaji Salama wa
Mitambo.
Mtendaji Mkuu Hadija, akasema pia kwamba kumekuwa na
ongezeko la upimaji afya za wafanyakazi kwa asilimia 163 kutoka
wafanyakazi 363,820 hadi wafanyakazi 955,959 waliopimwa katika kipindi
tajwa na kufafanua kuwa ongezeko hilo limetokana na kukukua kwa uelewa
miongoni mwa wadau, matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kutoa huduma za
usalama na afya ambayo imerahisisha upatikanaji wa huduma pamoja na
kuimarika kwa uwezo wa taasisi wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment