Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera Julius kalanga Laizer akiongea katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili 2023/2024.
Na Lydia Lugakila, Karagwe
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera Julius kalanga Laizer ametangaza msako mkali wa nyumba kwa nyumba kitanda kwa kitanda unaolenga kuwakamata Wazazi na walezi wa watoto ambao hawapeleka watoto shule
Laizer ametangaza kuanza kwa msako huo katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Angaza uliopo mjini Kayanga Wilayani Karagwe.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa tayari siku kumi na nne zimemalizika kwa mujibu wa sheria hivyo msako huo hautakuwa na huruma kwa mzazi au mlezi ambaye hadi Sasa hajampeleka mtoto shule kwani kwa kufanya hivyo ni kuhujumu haki ya mtoto.
"Natoa wito kwa Viongozi wetu wote kuanzia madiwani,vwatendaji wa kata, Waratibu Elimu kata, watendaji wa Vijijini, vitongoji, Viongozi wa dini na mabalozi na Chama hakikisheni tunapata taarifa kwenye Ofisi za serikali kwa watoto wote ambao wako nyumbani mpaka sasa"alisema Dc Laizer.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa Ameongeza kuwa kuanzia siku ya Jumatatu Januari 29, mwaka huu kwa siku nzima utafanyika msako wa kuwakamata Wazazi.
Amesema tayari serikali umeweka Mazingira mazuri ambapo hakuna mzazi anayedaiwa chochote ambapo watoto wengine wamelipoti wakiwa hawana viatu wala sare ya shule.
Ameongeza kuwa inatosha na umeishachorwa mstari hivyo hawatamvumilia mzazi yeyote au mlezi huku akiahidi watakaokamatwa dhamana yao itakuwa ni mtoto kuonekana na kupelekwa shule ambapo msako huo utafanywa zaidi ya mara kumi.
Hata hivyo Ameongeza kuwa hadi sasa 70% ya Wanafunzi ndio wamelipoti na 30% ambao ni sawa na Wanafunzi 2,000 bado wako nyumbani.
No comments:
Post a Comment