NA VICTOR MASANGU, PWANI
Serikali
Mkoani Pwani katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia
Suluhu Hassan imeweka mikakati kabambe ya kutenga maeneo kwa ajili ya
kilimo cha kisasa na chenye tija ambacho kitajumuisha mazao ya
kibiashara kwa lengo la kukuza uchumi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge wakati wa halfa fupi ya kukabidhi matreka matatu kwa uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha vijijini.
Kunenge
alisema kwamba matreka hayo matatu ambayo wamepatiwa na Rais Samia
yatakwenda kuwa msaada mkubwa na kuleta mapinduzi katika kilimo cha
kisasa.
"Sisi kama Mkoa
wa Pwani kwa sasa tumejipanga kuhakikisha kwamba tunajikita zaidi katika
kuboresha sekta ya kilimo na kwa sasa tumepokea matreka haya kwa ajili
ya halmashauri ya Wilaya ya Kibaha vijijini kwa hivyo hatuna budi
kumshukuru Rais wetu kwa hatua hii ya kutupatia matreka haya,"alisema
Kunenge.
Aidha Kunenge
alibainisha kwamba kwa sasa wameshaanza kujikita katika kilimo cha mazao
ya biashara ikiwemo zao la Pamba,ufuta kilimo pamba.mchikichi,korosho
mihogo pamoja na mazao mengine ambayo yataweza kuleta mabadiliko katika
kukuza shughuli mbali mbali za kiuchumi.
Aidha
aliongeza kwamba Mkoa wa Pwani wanataka kufanya mabadiliko makubwa
katika sekta ya kilimo hivyo ana imani kubwa mabadiliko hayo yatakwenda
katika halmashauri zote tisa zilizopo katika Mkoa wa Pwani.
Pia
kunenge aliwaomba viongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha kwamba
wanayatunza vizuri matrekta hayo ili yaweze kudumu kwa kipindi kirefu
ili kuweza kuwasaidia wakulima katika kilimo cha biashara.
Aidha
pamoja na hayo aliongeza kwamba katika kuendana na kasi ya mabadiliko
katika Wilaya ya Rufiji tayari kumeshafanyika uzinduzi wa zao la pamba
na kwamba kutajengwa kiwanda kikubwa kwa ajili ya kuchakata zao hilo.
Kunenge
amempongeza kwa dhati Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za
hali na mali katika kukuza sekta ya kilimo cha kuwezesha matreka hayo.
Aidha
Kunenge katika hatua nyingine aliwawahimiza wakulima wa Mkoa wa pwani
kuendana na mabadiliko na kuwataka wakulima wajikite zaidi katika kilimo
cha mazao ya biashara.
Sambamba
na hayo alisema wapo katika mikakati ya kujenga skimu kubwa za
umwagiliaji ambazo zitaweza kuwasaidia wakulima katika kuendesha
shughuli zao za kilimo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon amesema kwamba
wameshakubaliana matrekta hayo yatakwenda katika halmashauri ya Wilaya
ya kibaha ili kuboresha kilimo cha kisasa.
Aidha
alibainisha kwamba katika mpango wao wamekubaliana mambo matatu ikiwemo
kuunganisha kilimo pamoja na viwanda,rasirimali watu pamoja na
teknolojia lengo ikiwa ni kuwasaidia wakulima kulima kilimo cha kisasa.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha vijijini Erasto Makala
lengo lao kubwa ni kutoka katika kilimo cha chakula na kujikita katika
biashara.
Mkoa
wa Pwani kwa sasa umejipanga kuunganisha kilimo pamoja na viwanda lengo
ikiwa ni kutimiza azma ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hasssan kulisha dunia
nzima kupitia sekta ya kilimo.
No comments:
Post a Comment