Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na timu ya Menejimenti ya Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) ambapo amewataka kuja na ubunifu wa kujenga makazi bora ya watumishi wa umma katika maeneo ya mijini jirani na maeneo ya shule na hospitali ili kuwaondolea changamoto ya makazi manesi na walimu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameitaka Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) kuja na ubunifu wa kujenga makazi bora ya watumishi wa umma katika maeneo ya mijini jirani na maeneo ya shule na hospitali ili kuwaondolea changamoto ya makazi manesi na walimu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao
Amesema
maeneo ya mijini, shule pamoja na hospitali zinamiliki maeneo makubwa
ambayo Taasisi ya WHI inaweza kuyatumia kujenga majengo marefu kwenda
juu ili kuwafanya walimu na manesi wafurahie kutoa huduma kwa wananchi
kwa kuishi kwenye makazi bora jirani na maeneo ya kazi
Mhe.
Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa
akizungumza na Timu ya Menejimenti ya Taasisi ya Watumishi Housing
Investments (WHI) ikiwa ni muendelezo wa kusikiliza changamoto
zinazoikabili Taasisi anazozisimamia pamoja na kufuatilia utekelezaji
wa maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara aliyoifanya Mwezi Agosti mwaka
jana
Amesema
katika maeneo ya mijini watumishi wakiwemo walimu na manesi wamekuwa
wakilazimika kutafuta makazi mbali na maeneo wanakofanyia kazi kwa vile
ni vigumu kupata nyumba karibu na maeneo hayo na hata makazi
yakipatikana gharama zake za kulipia huwa ni kubwa kulingana na kipato
chao.
'' Hakuna asiyejua umuhimu wa
walimu na manesi katika nchi hii lakini lakini wengi wa wamekuwa
wakiishi maeneo ya mbali na wanakofanyia kazi na hivyo kulazimika kulipa
nauli kubwa kwa vile hawawezi kumudu kulipa kodi ya makazi yaliyo
jirani na maeneo yao ya kazi, waguseni hawa kwa kuwajengea makazi bora.
amesema Mhe. Simbachawene
Mhe.Simbachawene
amesisitiza kuwa Nyumba zikiwa jirani na eneo la kazi inasaidia
kupunguza gharama za maisha na kuongeza ufanisi kazini na hilo ndio
lengo haswa la Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha watumishi
wanafurahia mazingira ya kazi kwa gharama rafiki"
Amesema
Watumishi wa Umma wakiwemo walimu na manesi wanaofanya kazi katika
maeneo ya mijini wamekuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kutokana na
changamoto ya makazi na hivyo kupelekea kutoa huduma zisizoridhisha kwa
wateja wao.
Mhe.
Simbachawene amesema kitendo cha watumishi wa umma kutokuwa na makazi
bora na kuwa mbali na maeneo yao wanayofanyia kazi ni changamoto kubwa
inayoathiri utendaji kazi, hivyo ameitaka taasisi hiyo kuona umuhimu wa
kufanya hivyo kwani utekelezaji wq ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya
mwaka 2020/ 2025
Mhe.
Simbachawene amesema ujenzi wa makazi bora hayo karibu na maeneo ya
kazi, kutawasaidia watumishi wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza maeneo
kutohangaika. “Mkijenga nyumba maeneo ya jirani na vituo vya kazi,
kutawasaidia sana watumishi kutoichukia kazi kwa watapata sehemu nzuri
ya kuishi,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Kwa
upande wake Mkurugezi wa Taasisi ya Watumishi Housing, Dkt.Fred
Msemwa amesema kwa mwaka 2023/ 24 imeendelea na ujenzi wa nyumba
Njedengwa, Magomeni na Gezaulole lengo likiwa ni kupunguza adha
wanazozipata watumishi wa umma wakiwemo walimu na manesi
No comments:
Post a Comment