Kwa taarifa hii, tunapenda kuujulisha umma kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu haiitambui Taasisi hiyo, na wala Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa haitambui na hajawahi thibitisha popote uhalali wa Taasisi hiyo.
Ofisi ya Waziri Mkuu inautaarifu umma kuwa Serikali inao utaratibu wa mikopo kwa wananchi kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Hivyo wananchi wanao hitaji kupata taarifa za mikopo ni vyema kufika katika Idara za Maendeleo ya Jamii zilizopo katika Halmashauri zote nchini pamoja na Ofisi za Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi.
No comments:
Post a Comment