HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 29, 2024

RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSANI KUFANYA ZIARA NCHINI KOREA KWA SIKU 6

Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam

Rais  wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt samia suluhu hassani anatarajia  kufanya  Ziara ya kikazi Nchini korea siku sita kuanzia Mei 30,2024.



Akitoa taarifa hiyo leo Jijini Dar es salaam Mei 29,2024 Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba amesema   ziara hiyo italeta tija kwa Tanzania kwani Serikali itaingia Mkataba wa wa Msaada wa mkopo nafuu wa Dola za Kimerekani 2.5 bilion sawa na shilingi 5.2 trilion kutoka serikali ya Korea fedha hizo zikienda katika sekta  ikiwemo Elimu, Afya, na miundombinu .

Makubaliano haya ni mapya ya Ushirikiano wa maendeleo kati ya Serikali ya Tanzania na Korea na Mkataba huu ni mkubwa kati ya saba itakayoingia Juni 2,2024 kati ya Taifa hili na nchi hiyoo" amesema Waziri

Sanjari na hayo Rais Dkt samia Suluhu Hassan atafanya mazungumzo na kusaini mikataba saba ya ushirikiano
 kati ya Tanzania na Korea  na  Hati ya makubaliano kati ya Taasisi ya Madini Tanzania. GST na Taasisi ya miamba nchini korea ushirikiano  kuhusu utafiti, uchoraji ramani, rasilimali na uchoraji  wa maabara .

Pia Mkataba wa pili ambao unaenda kusainiwa kati ya Rais Samia na Rais wa korea ni ushirikiano wa uchumi huku mkataba wa tatu ukihusu kwenda kutambua vyeti vya Mabaharia  pia  wataweza kusaini  Tamko la pamoja kuhusu siasa  na makubaliano ya hati ya Madini, Viwanda na biashara  

Aidha  Waziri  Makamba ameongeza kuwa kuhusu madini kwenye mkakati watasaini  mkataba katika kuwezesha  kuchambua, na kufanya Mkakati na shirika la madini   Tanzania  STAMICO ,  na shirika la ukarabati  wa madini nchini korea.

Hata hivyo Mkataba mwingine ni Msaada wa fedha kutoka benki ya Exim nchini korea  na serikali ya  Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao unaenda kupelekea nchi yetu  kupata msaada    na mikopo nafuu Takribani dola mbili nanusu vilevile  wataenda kushirikiana na chuo kikuu kutoka nchini korea katika kuendeleza huduma za usafiri wa anga nchini

No comments:

Post a Comment

Pages