HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 09, 2024

TCB Bank yazindua Toboa na Vicoba, Vikundi vya Kijamii sasa Kidigitali

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Mihayo (katikati), akizindua Kampeni ya Toboa na Kikoba kwa ajili ya kuweka na kukopa, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 9, 2024.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), wakiwa katika uzinduzi wa Kampeni ya Toboa na Kikoba kwa ajili ya kuweka na kukopa, hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 9, 2024.




Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Mihayo (katikati), akikata keki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Toboa na Kikoba kwa ajili ya kuweka na kukopa, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 9, 2024.
 


NA MWANDISHI WETU
 

BENKI ya Tanzania Commercial Bank (TCB Bank), imezindua Kampeni ya Toboa ana Vicoba, huduma itakayowawezesha Watanzania hasa wanachama wa Vikundi vya Kijamii vya Akiba na Mikopo, kufanya miamala kidigitali.

Uzinduzi wa huduma hiyo inayolenga kuunga mkono jitihada za Serikali kuongeza idadi ya Watanzania walio kwenye mnyororo wa thamani wa Huduma Jumuishi za Kifedha, umefanyika jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Mei 9.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TCB Bank, Adam Mihayo, alisema benki yake ambayo inapewa ruzuku na Serikali, imeona ipo haja ya kusapoti jitihada hizo kwa kubuni bidhaa inayogusa Watanzania walio wengi.

“Kampeni ya Toboa na Vicoba inalenga kuwajulisha Watanzania aina ya ubunifu tulionao kwa kushirikiana na kampuni za simu, ambapo tumekuja na ufanisi ambao utawawezesha kufanya miamala ya Vikundi vya Akiba na Mikopo kisasa zaidi.

“TCB ni benki Inayomjali na Kumuelewa Mteja, na katika tafiti zetu tumegundua ‘life style’ ya Watanzania walio wengi inajumuisha Vikundi vya Kijamii, walivyounda huko makanisani, misikitini, katika koo zao na wengi walikuwa wanafanya kienyeji.

“Sisi tukaona kuna haja ya kuongeza usasa, ndipo tukabuni Toboa na Vicoba kuwawezesha kufanya miamala ya vikundi kidijitali kupitia ‘platform’ hii yenye kuwezesha kufanya miamala hiyo kirahisi na kwa usalama, huku kila mwanachama akijua na kuona.

“Lakini dhumuni kubwa ni kuongeza ujumuishwaji wa kifedha, kwani takwimu zinaonesha Watanzania wanaotumia huduma za kibenki ni asilimia 23 tu.

“Tukaona kwa kushirikiana na kampuni za simu, tunaweza kusukuma mbele ajenda hii ya Serikali ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki,” alibainisha Mihayo na kuongeza kuwa huo ni mwanzo tu, matarajhio yao ni kuwa na huduma nbyingi zaidi kidijitali.

Alibainisha ya kwamba, TCB ni benki ya Serikali yenye matawi 82 - inayofuata maelekezo na miongozo ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hivyo inalo jukumu la kushirikiana nayo katika kupeleka mbele ajenda zote za kimkakati.

“Kampeni hii itaenda nchi nzima kuwaelewesha Watanzaia namna ya kunufaika na Toboa na Vicoba, huduma chanya, rahisi, nafuu na salama zaidi kwa ustawi wa vikundi vyao, wanachama mmoja na taifa kwa ujumla,” alisema na kuwataka Watanzania wachangamkie huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages