HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2024

DK. BITEKO AIPONGEZA TMA KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA UTABIRI WA HALI YA HEWA

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko, ameipongeza Mamalaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kuendelea kutoa huduma bora za hali ya hewa nchini.


Amesema hayo wakati alipotembelea banda la TMA kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani, yanayo fanyika katika viwanja vya JICC, mjini Dodoma.

Dk. Biteko alikuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa maadhimisho haya muhimu kwenye ukuaji wa sekta ya mazingira nchini na alitembelea banda la TMA na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a.

“Hongereni sana kwa huduma bora za utabiri mnazotoa kila siku na zinatusaidia sana, hongereni sana, amesema Dk. Biteko.

Kwa upande wake Dk. Chang’a aliwaomba wananchi wa Dodoma na wale wa mikoa ya jirani watumie fursa hii kwa kutembelea banda la TMA kwenye maadhimisho haya ili kujifunza masuala mbalimbali ya mazingira na huduma zitolewazo na TMA.

 “Karibuni wananchi wote katika banda la TMA, mje kujifunza na kuongeza uelewa wa huduma za hali ya hewa na matumizi yake katika sekta zote za kiuchumi na kijamii. Mtajifunza uhusiano wa hali ya hewa na mazingira yanayotuzunguka.

"Tunao wataalam bingwa wa hali ya hewa na wapo tayari kutoa elimu kwenu," amesema Dk. Chang’a.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inashiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya wiki ya Mazingira kwa mwaka 2024 yenye kauli Mbiu "Urejeshwaji wa Ardhi, Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na Ukame"

No comments:

Post a Comment

Pages