HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 12, 2024

MAGEUZI YA MASHIRIKA YA UMMA NI CHACHU YA MAENDELEO

Na Mwandishi Wetu


Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan akipokea  gawio kutoka mashirika na taasisi za umma na kampuni ambazo Serikali ina Hisa chache, Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu amesema mageuzi ya mashirika ya umma ni chachu ya maendeleo ya Taifa.


Ameyesema hayo katika hafla hiyo ambayo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema uchangiaji upo katika namna mbili ya kwanza ni kwa taasisi za biashara ambazo zinatakiwa kutoa sehemu ya gawio la faida kwa wanahisa wake.


"Mheshimiwa Rais, Kauli mbiu ya zoezi hili la gawio kwa mwaka huu ni “mageuzi ya mashirika ya umma na wajibu wa kuchangia maendeleo ya Tanzania”.

Kauli mbiu hii tumeiweka kuakisi umuhimu wa kuimarisha utendaji
kazi katika mashirika na sehemu zote zenye uwekezaji wa Serikali na
pia kutimiza wajibu wao wa kuchangia maendeleo ya nchi yetu kupitia
gawio na michango ambao ni zao la uwekezaji uliofanywa na Serikali." amesema Mchechu.

"Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Nasimama hapa ikiwa ni mara yangu ya kwanza kuambatana na viongozi wa taasisi zote hizi kuja kuwasilisha gawio la ujumla kwako kutoka katika mashirika na taasisi zote ambazo Serikali ina uwekezaji tangu uniteue kuwa Msajili wa Hazina. Ninaelewa kuwa mwaka 2023 niliwasilisha gawio kutoka kwa taasisi moja. Hata hivyo, tofauti na mwaka jana, mwaka huu tumeona tuanze utamaduni wa kuyaleta
mashirika pamoja na kufanya matukio ya msingi kwa pamoja.


"Utamaduni wa kwenda pamoja tunautimiza kama ulivyoagiza tarehe 11
Disemba 2023 wakati tulipowasilisha michango ya mashirika ya umma
kwenye kusaidia janga la maporomoko ya Hanang. Ni ahadi yetu kuwa
tutaendeleza umoja huu kwa maslahi mapana ya nchi yetu." Amebainisha kuwa.

"Kwanza, ofisi ya msajili wa hazina imeendelea kushawishi
kufanyika kwa reforms katika sheria yake ili kuanzishwa kwa mamlaka ya uwekezaji wa umma. Kwa hatua tuliyofikia, naomba nimshukuru Waziri wetu Profesa Kitila Alexander Mkumbo kwa kujitoa kwake na ari aliyoionesha kwenye kuandaa na kuhakikisha muswada huu unapita
kama ulivyoelekeza.

Ni imani yetu, baada ya muswada kusomwa kwa
mara ya kwanza Novemba 2023 utaendelea na hatua zinazofuata. Aidha
tunaamini tupo kwenye njia sahihi ya kuhakikisha mabadiliko
yanafanikiwa kupitia sheria mpya ya mamlaka ya uwekezaji wa umma.
Ni wazi kuwa tunahitaji sheria inayojitosheleza itakayoweza kusaidia
kuleta tija katika uwekezaji mkubwa wa zaidi ya TZS 76 Trilioni
uliofanywa na Serikali kwa niaba ya Umma wa Watanzania.

La pili, Msajili wa wa hazina imefanya mkutano na mafunzo kwa
wakurugenzi wanaotuwakilisha kwenye kampuni ambazo tuna umiliki
wa hisa chache. Mafunzo haya yalikuwa na umuhimu mkubwa chini ya
kaulimbiu ya “Uzalendo wa Kiuchumi katika uwekezaji wa Umma”.

Sehemu ya matokeo ya tutakachokiona leo ni matokeo ya mafunzo
haya. Pia tumeendelea na mafunzo ya Wakurugenzi wa Bodi kwenye
Mashirika ya Umma kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi. Na
kuanzia mwaka ujao wa fedha tutaanza na mafunzo maalum (Induction
Course) kwa kundi la Watendaji Wakuu wapya walioteuliwa ndani ya
kipindi cha miaka miwili kama sehemu ya kuimarisha utendaji kazi wa
mashirika haya.

La tatu, katika kuimarisha utawala bora na tija ya mashirika ya
umma, Ofisi imezindua na kuanza kutumia mfumo wa kidijitali wa
kufanya tathmini ya bodi hali ambayo imewezesha kukamlisha
tathmini kwa wakati na kwa mawanda tarajiwa.

Aidha  amesema "Ofisi imeanza kutumia vigezo vipya vya uendeshaji wa mashirika (Key Performance Indicators) vilivyoingiwa kwa njia ya mikataba baina ya wenyeviti wa Bodi na Msajili wa Hazina. Vigezo hivi vimeboreshwa zaidi na vimezingatia mgawanyo wa kisekta na majukumu ya msingi ya taasisi, na tutaendelea kuboresha vigezo hivi mara kwa marana pia kwa
kutegemea mrejesho kutoka taasisi zetu hizi ambao ndio wadau wetu.

La nne, tupo katika hatua za mwisho za kuwa na mfumo thabiti
wa kuripoti (dashboard) taarifa za kiutendaji za wakuu wa taasisi kwa
wakati na za kuaminika ili kuwezesha kufanyika maamuzi sahihi kwa
wakati (informed decision making) kwa mamlaka za uteuzi.
Ofisi pia imefanikiwa kupitia mikataba mbalimbali ya kibiashara
na pia kufanya mazungumzo na wabia wetu kwenye sekta nyeti za
Uchumi; kwenye sekta ya madini kumekuwa na mzungumzo
mbalimbali tukishirikiana na Wizara ya Madini na tumeweza kuongeza
hisa za serikali katika baadhi ya Kampuni, Mathalani tumeongeza hisa
za serikali katika Kampuni ya madini ya Sotta kutoka 16% hadi 20%,
jambo litasaidia sana katika majadiliano ya mikataba mingine ambayo
tupo katika mazungumzo.

Pia tumekamilisha majadiliano na kuingia
mipya ya wanahisa na makampuni kama NMB, NBC na MCCL kati ya
mikataba mingi inayofanyiwa kazi, na kampuni ya MCCL imeweza
hatimaye kupata faida mwaka huu na kutoa Gawio kwa wanahisa
Mwaka huu baada ya kipindi cha miaka 10."amesema Mchechu

No comments:

Post a Comment

Pages